TARURA KUJENGA BARABARA ZA LAMI KILOMITA 427 MWAKA HUU

 ðŸ“ŒSUZANA ALEX

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  imepanga kutumia sh.bilioni 858.5 kwa ajili ya kutengeneza  barabara zenye urefu wa kilomita 21,058, kujenga kiwango cha lami kilomita 427 na kujenga makalavati na madaraja 855 katika mwaka huu wa fedha.

Pia, imepanga kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 8,775 kwa kiwango cha changarawe na ujenzi wa mifereji ya mvua yenye urefu wa kilometa 70.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma leo, na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi  Victor Seff wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa taasisi hiyo na mwelekeo katika  mwaka huu wa fedha.

Katika mwaka huu wa fedha  Barabara zenye kilomita 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo, kilometa 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, kilomita 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa na mifereji ya mvua km 70

Ameongeza kuwa Jumla ya sh. bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za Wilaya.

Amefafanua kuwa  kati ya fedha hizo, sh. bilioni  710.31 ni fedha za ndani na sh. bilioni  148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na mradi wa Agri connect.

Mhandisi Seff amebainisha kuwa  hadi sasa TARURA imetangaza kazi za ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara zaidi ya asilimia 60 ya mpango wa mwaka huu wa fedha  ambapo baadhi ya kazi utekelezaji umeanza.



 

Post a Comment

0 Comments