TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kudhibiti shilingi milioni 3.9 fedha za
wanufaika wa TASAF zaidi ya 130 walizokatwa kwa madai ya kupewa bima ya afya.
Hayo yamebainishwa leo Jijini dodoma na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma John Joseph wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji majukumu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2023.
Baada ya TAKUKURU kupata taarifa na kuingilia kati mtumishi huyo amerejesha fedha hizo na tayari zimewasilishwa katika mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya wanufaika hao 130 wa mfuko wa TASAF katika akaunti ya mfuko wa Afya Dodoma Namba 50510042226
Joseph.
Aidha Mkuu huyo aliendelea kwa kusema katika kipindi cha miezi mitatu April hadi Juni 2023 wameweza kufanya kazi za uzuiaji rushwa kupitia uchambuzi wa mifumo, ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo na udhibiti wa vitendo vya rushwa kupitia programme ya TAKUKURU Rafiki vilevile wameweza kufanya uelimishaji wa jamii kupitia mbinu mbalimbali za uelimishaji pia kufanya uchunguzi wa makosa ya rushwa yaliyobainika.
Pia ametoa wito kwa kusema kila mmoja wetu kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa ni wajibu wa kikatiba kwa kila mmoja wetu [Ibara ya 9(H)], pamoja na kuwa ni wajibu wa kikatiba pia ni jambo la kiimani kwani maandiko matakatifu kutoka katika Vitabu Vitakatifu yaani Biblia na Quran vyote vinakataza vitendo dhidi ya Rushwa na Maandiko yameonyesha wazi kuwa kila anayejihusisha na Rushwa amelaaniwa na Mwenyezi Mungu [Ayubu 15:34-35, Ezekiel 22:12-16 na Suurat Bagarah Aya ya 188]
Niwashukuru wanaDodoma wote ambao wamekuwa na wanaendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na kwa aina ya pekee sana niwapongeze waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari ambavyo vimeendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa jamii na baadhi ya vyombo hivyo vimekuwa vikitupatia nafasi kila wiki ya kutoa Elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa jamii bila malipo ya aina yoyote,huu ni moyo wa kizalendo, moyo wa kulipenda taifa niwaombe muendelee na uzalendo huu bila kuchoka pia nitoe wito kwa vyombo vingine kuiga moyo huu wa kizalendo
Joseph.
0 Comments