SERIKALI YA AWAMU YA SITA KUHAKIKISHA VIJANA ,WANAWAKE WANAJIKITA KWENYE KILIMO

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pindi Chana  amesema kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wanawake na vijana wanachangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo .

Pia ni ajenda ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na baadae kusambaza duniani kote.

Waziri Pindi ameyasema Jijini hapa katika ufunguzi wa kongamano la zao la mtama maonyesho ya wakulima 88 Nzuguni Dodoma wakati alipotembelea moja ya shamba la mahindi na kuwasihi wananchi haswa wanawake na vijana kuchangamkia fursa za kilimo ikiwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania.

Nimeambiwa kuwa haya ni Maonesho ya Kumi na Tano ya Kanda na Maonesho ya kumi na mbili ya Mashindano ya Mifugo Kitaifa yatafanyika mwaka huu.

Waziri Chana

Aidha amesema kuwa sekta ya Kilimo inayojumuisha Mazao, Mifugo, Uvuvi na Misitu bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania, kwa sababu inaajiri zaidi ya asilimia 80 ya watanzania na kwa kuzingatia Malengo ya Maendeleo ya Taifa ya kuwa nchi yenye Uchumi wa kati unaotegemea Viwanda.

Ninaamini Kilimo kikiboreshwa viwanda vyetu vitapata malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima wetu, hivyo kuwepo kwa ajira za kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla

Wastani  wa ukuaji wa Sekta ya Kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na kilimo chetu kwa kiwango kikubwa, kutegemea Mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa viwango na mtawanyiko unaotofautiana mwaka hadi mwaka. Kwa mwaka 2022 Sekta ya Kilimo ilikua kwa asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwaka 2020

Chana

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Selukamba amesema kama mkoa zao lao la kimkakati ni alizeti na  mpaka sasa wamefikia asilimia 44% ya uzalishaji na kusambaza mikoa ya jirani ikiwemo Dodoma na Manyara na ni zao ambalo linawainua wananchi kiuchumi.

Mikoa ya Dodoma na Singida ni maarufu kwa kilimo cha zao la mtama wa aina mbalimbali. Umaarufu huu, umechangiwa na hali ya hewa inayopatikana maeneo mengi ya mikoa hii kustawisha vizuri zao la mtama.

Kwa muktadha huo, Mtama ni zao linalohimizwa kuzalishwa kwa ajili ya uhakika wa usalama wa chakula na kipato kufuatia kuongezeka kwa uhitaji wa zao hili hapa nchini na nchi Jirani kama Burundi, Ruanda, Southern Sudan na Kenya

Selukamba

Hata hivyo maonesho hayo yanabebwa na kauli isemayo "VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA"

 

Post a Comment

0 Comments