SERIKALI IMEJIPANGA KUREJESHA MISITU YA MIOMBO


📌AISHA SULEYMAN

DODOMA. Serikali imesema kuwa imejipanga vizuri kurejesha hifadhi ya misitu ya miombo kwenye Nyanda za Mlele na Kaliua ili kurejesha uoto wa asili wa misitu hiyo ambayo imeathiriwa  na uharibifu wa mazingira.

 Hayo yalibainishwa Jana na mratibu wa mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu ya miombo Tanzania, Zainabu Bungwa kwenye kikao cha awali cha wataalam wa mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu ya miombo ya Nyanda kame Jijini hapa. 

Bungwa amesema misitu ya miombo inabeba asilimia 90 ya misitu yote iliyopo nchini hivyo uharibifu wake unaathiri eneo kubwa la ardhi nchini.

Amesema wameamua kuweka nguvu kubwa kwenye urejeshwaji wa misitu hiyo ambayo imeathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kwenye vijiji vinavyozunguka misitu hiyo ili kunusuru uharibifu wa mazingira nchini.

Lengo letu kubwa ni kunusuru na kupunguza uharibifu wa misitu ya miombo inayoendelea lakini pia kujibu matokeo ya kidunia yanayoitaka kila nchi kupunguza uharibifu wa ardhi kutoka asilimia 90 hadi asilimia 0

Bungwa.

Amesema mradi huo upo kitaifa ambapo utanufaisha pande zote zinazozungukwa na misitu hiyo kwa upande wa Halmashauri na upande wa wanakikjiji wanaotegemea hifadhi hizo kwa ajili ya shughuli zao za kila siku

Amesema katika mradi huo watatekeleza shughuli mbadala au sahihi ambazo zinatakiwa kuwanufaisha wananchi wanaoishi kwenye mazingira yale ili waachane na shughuli za kuharibu mazingira kwenye misitu hiyo

Kutakuwa na usimamizi shirikishi wa matumizi bora ya ardhi ambazo zitawawezesha wananchi kupata shughuli mbadala na sahihi za kujipatia kipato kwenye upande wa uzalishaji na mnyororo mzima wa asali pamoja na huduma mbalimbali zitokanazo na misitu ya miombo

Misitu ya miombo inachukua asilimia 90 ya misitu yote Tanzania lakini pia jamii inayoishi kwenye mazingira yake inategemea asilimia 90 ya maisha yake kwenye misitu hiyo.

Amesema uharibifu wa mazingira nchini ni asilimia 61 huku uharibifu huo ukiwa ni hekta 469,000 kila mwaka huku misitu inayoongoza kwa uharibifu ni ile inayomilikiwa na serikali ya vijiji na ile ya watu binafsi.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi mkuu wa utafiti wa misitu Tanzania (TAFORI) Dk Revocatus Mushumbusi amesema lengo kuu la mradi huo ni kukomesha na kubadili mwelekeo mbaya wa uharibifu wa ardhi na upotevu wa bioanuwai katika maeneo yaliyoharibiwa ya ukanda wa Misitu ya Miombo Kusini-magharibi mwa Tanzania kwa kutumia mbinu shirikishi za usimamizi wa mandhari.

Dk Mushumbusi amesema mradi huo unatekelezwa katika nchi 11 ambapo mwisho wa siku kila nchi itapimwa kwa matarajio waliyojiwekea ambapo Tanzania itapimwa kwa uhifadhi mzuri wa misitu ya miombo na hatimaye kuleta tija kwenye mnyororo mzima wa mazao ya nyuki na maisha ya jamii.

Sambamba na ukubwa huo changamoto za uharibifu wa ardhi, uharibifu wa ikolojia ya Misitu ya miombo ya Nyanda kame, kupungua kwa bioanuwai muhimu ni mkubwa na hivyo kupungua kwa huduma zitokanazo na ikolojia hiyo unazidi kuongezeka hasa ukizingatia changamoto za kilimo cha kuhamahama, mifugo iliyo kwa makundi makubwa, ukataji na uharibifu wa misitu kwa ajili ya nishati ya mkaa

Dk Mushumbusi .

Amesema changamoto hizo kwenye ardhi ya misitu ya miombo inazidi kuongezeka ikiwa ni pamoja na ukame unaozidi kuongezeka na mabadiliko ya tabianchi kwa nchi na dunia nzima.

                                   

 

 

Post a Comment

0 Comments