WAKALA wa nishati vijijini (REA) umeendelea kuhamasisha na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini katika maeneo mbalimbali na mikoa yote ya Tanzania bara ili kuwafikishia huduma wananchi wengi zaidi vijijini.
Miradi hii ni pamoja na kuongezea wigo wa Grid ya Taifa (grid extension) kufikia kwenye vijiji na vitongoji vyote nchini na miradi ya nje ya grid (off grid) ikijumuisha mifumo midogo ya uzalishaji wa umeme yaani Renewable energy source.
Mradi huu unahusisha kupeleka umeme kwenye vijiji 4071 vilivyobaki kati ya Vijiji vyote 12,318 pamoja na kujenga njia za umeme wa msongo wa kati zenye urefu wa kilometa 23,526 na kujenga njia za umeme wa msongo mdogo zenye urefu wa kilometa 12159 na kufunga mashine umba 4071
Kuunganisha wateja wa awali wapatao 258,660. Mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bank ya dunia kwa kiasi cha shilingi trilion 1.58 kwa sasa mradi huu upo katika hatua ya utekelezaji ambapo unatarajiwa kukamilika Disemba 2023 kwa mikataba 32 na Juni 2024 kwa mikataba Saba (7) utekelezaji wa miradi huu kwa sasa umefikia asilimia 73
Aidha mradi huu unahusika kupeleka umeme katika maeneo 114 ya wachimbaji wadogo wa madini maeneo 222 ya viwanda na kilimo katika mikoa 25 ya Tanzania bara.
Serikali kupitia (REA) imewapata wawekezaji watu(3) kwa mradi wa kusambaza umeme kwa kupitia nguvu ya jua itakayotekelezwa katika visiwa 28 vilivyo Katika mikoa ya Kagera (8), Mwanza (13), Mara (3) Lindi (4) na hivyo kuunganisha wateja 9515 kwa gharama ya shilingi 11.18 bilioni
Mradii huu unajumuisha ujenzi wa miradi midogo na kusambaza umeme katika maeneo yenye vyanzo nishati ya kuzalisha umeme kwa kutumia mapolomoko ya maji ambapo mikataba miwili (2), miradi ya Ikondo Matembwe hydro power ulisainiwa February 2023 na mkataba wa Mwanga power ulisainiwa mwezi machi 2023.
Baada ya kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme vijijini serikali imepanga kusambaza umeme katika vijiji na vitongoji ili kuhakikisha umeme unafika katika maeneo yote ya Tanzania bara.
Serikali imepata mkopo wa gharama nafuu kutaka shirika la fedha duniani (IMF) kupitia dirisha la extended credit facility ambapo kiasi cha shilingi bilioni 100 itatumika kutekeleza mradi huu Katika vijiji na vitongoji vya Tanzania bara
REA na TANESCO wapo katika hatua ya mwisho ya kusaini makubaliano ambapo TANESCO utafanyaa kazi ya kupeleka umeme katika shule na mahakama na REA itatia fedha ya utekelezaji wa miradi hiyo.
0 Comments