Mgeni Rasmi RC Selukamba akiwa katika Banda la Mbolea FOMI |
KUELEKEA maazimisho ya siku ya wakulima
duniani tarehe 8 Agosti ya kila mwaka viwanja vya nanenane Nzuguni jijini
Dodoma, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Peter Selukamba
atembelea mabanda mbalimbali kwa lengo la ufanya uzinduzi wa maenyesho ya
wakulima Kanda ya kati Dodoma.
Akizungumzia maonyesho hayo mbele ya Mgeni Rasmi, Afisa Masoko wa kiwanda cha uzalishaji wa mbolea (ITRA COM), Janvier Sibomana ambao ni wazalishaji wa mbolea aina ya Fertilizer Organic Minerals Industries (FOMI) amesema mbolea hizo zipo aina tatu ambazo ni fomi otesha, kuzia na nenepesha pia amesema mbolea hizo zinatumika kwa awamu tofauti.
Amesema tofauti ya mbolea hiyo na zingine ni kuongezea mbolea za asili ikiwa na nia ya kuboresha ubora wa udongo wakati chumvi chumvi zinavuta chakula zinakiletea mimea wanakitumia lakini kilipotoka chakula hicho kunabaki wazi na mbolea ya asili ambayo hufahamika kama samadi huboresha udongo kwa kuweka unyevunyevu katika ardhi na kusaidia aridhi kuwa tifutifu.
Aina ya mbolea hii inatumika sana nyanda za juu kusini Mbeya, Ruvuma, Iringa kutokana na uhitaji wa mbolea hiyo hasa kwa mazao kama mahindi, maharage, viazi na alizeti pia mbolea hii ina uwezo wa kutumika maeneo yote ya Tanzania.
Kuna mbolea ambayo bado ipo kwenye majaribio ni mbolea ya chai kwasasa haijaingia sokoni pindi itakapo vunwa na tukaona ubora wa chai hiyo na ladha yake kama ni nzuri basi mbolea hio itaingia sokoni
Sibomana.
Sherehe hizi huazimishwa kila tarehe 8 Agosti ya kila mwaka na kitaifa mwaka huu maazimisho hayo yanafanyikia kitaifa jijini Mbeya.
0 Comments