PROF JANABI ATOA USHAURI KWA KLABU ZA LIGI KUU.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amezishauri klabu za Tanzania kuhakikisha zinawapima afya ikiwemo ugonjwa wa moyo wachezaji kabla ya kuwasajili.

Prof Janabi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 10, 2023 jijini Dodoma  wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na Mwelekeo wa Hospitali hiyo kwa mwaka  wa fedha 2023/2024 kwa Waandishi wa Habari.

Amesema anajua baadhi ya klabu zimekuwa zikisajili wachezaji kwa gharama kubwa bila ya kuangalia afya zao jambo ambalo ni la hatari.

Prof Janabi pia ameshauri wachezaji wanaoshiriki Jogging kuhakikisha wanapima magonjwa ya moyo kabla ya kuanza kukikimbia kwani kutokufanya hivyo ni hatari kwa afya zao.

Prof Janabi pia amelitaka Baraza la Michezo (BMT) kuweka mikakati ya kuwapima wachezaji wa michezo yote afya ikiwemo ugonjwa wa moyo.

Katika hatua nyingine  hospitali  hiyo  imeanza utaratibu wa kuwatumia waraibu wa dawa za kulevya ambao wameshapona  kwa kuwapa ajira mbalimbali ndani ya hospitali ili wasiweze kurudi tena kutumia dawa hizo.

Aidha, Prof, Janabi ameongeza kuwa mbali na huduma za matibabu ambazo wameendelea kuzitoa Hospitalini hapo wameanzisha utaratibu wa kutoza  tozo ya parking za magari kwa lengo la kuongeza mapato ya hospitali na kupunguza msongamano wa magari ambayo  mengi yameonekana sio ya Wafanyakazi wa Hospitali.

 


 

 

Post a Comment

0 Comments