MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony Mavunde
amewataka vijana kutumia michezo kama sehemu ya kujitafutia fursa ya ajira
badala ya kuwa burudani pekee.
Amesema hayo wakati akifungua awamu ya pili ya michuano ya Ndondo cup 2023 Mkoa wa Dodoma.
Msimu wa 2023 Ndondo cup Mkoa wa Dodoma unaingia msimu wa pili, hivyo tutakuja na utaratibu tofauti, nimewaomba wataalamu, makocha na walimu kuhakikisha wanafanya skauting ya wachezaji na kuunda kikosi cha wanaotokana na mashindano haya
Mavunde.
Aidha amesema
Mwakani tutaingia makubaliano na Netsport wanaotengeneza jezi za Dodoma Jiji, watazalisha jezi kwaajili ya timu za Ndondo cup msimu ujao huku kila timu shiriki ikipata jezi bure na zawadi msimu huu zikiongezeka
Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo, Yahaya Mkazuzu, amesema Ndondo cup ilianzishwa 2014 na kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dodoma ukitoa Dar es Salaam ambao ndio Mkoa muasisi.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Dodoma (Dorefa), amesema viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Central Sekondari-mtekelezo, Sheri complex - Maili Mbili na Chang'ombe Gwasa ambapo hakutakuwa na kiingilio na kutarajiwa kuanza Septemba 10, mwaka huu.
Aidha Afisa habari wa Chama cha soka Mkoa wa Dodoma Timothy Francis amesema timu yoyote itakayojisajili italipa ada ya shilingi laki tatu.
0 Comments