MOI YATENGEWA BILIONI 55.9 KUBORESHA TIBA NA UENDESHAJI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) Profesa Abel Makubi amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga jumla ya Sh 55.9 bilioni kwa Taasisi hiyo kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba na shughuli za uendeshaji.

Ameyasema hayo leo, Agosti 3, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita na Mipango ya mwaka 2023-2024 kwa waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.

Amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023-2024 Serikali imetenga jumla ya Sh 55.9 bilioni kwa Taasisi hiyo ili kuboresha huduma za tiba na shughuli za uendeshaji

Profesa Makubi ameitaja mipango ya MOI ni pamoja na kuongeza ubora wa huduma zote ndani ili kukidhi matarajio ya wananchi ndani ya nchi na kufikia viwango vya Kimataifa.

Pia kuanzisha huduma mpya tatu za kibingwa na kibobezi ambazo bado zinasababisha rufaa nje ya nchi (Tiba ya baadhi ya Kiharusi kupitia Angio-suite, Tiba ya baadhi ya vifafa kupitia upasuaji na upasuaji wa kiuno kwa njia ya matundu (Hip arthroscopy).

Ameitaja mipango mingine ni ukarabati wa miundombinu ya Hospitali Ujenzi mpya wa  miundombinu, ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo litakuwa na vyumba 30 vya kliniki vya kisasa tofauti na vyumba 7 vilivyopo sasa.

Pia Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao, mazoezi ya viongo na upasuaji wa mifupa (Rehabilitation and Spine centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji Mbweni jijini Dar es salaam.

Kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana muda wote ambapo zimetengwa TZS bil 2 kwa mwaka huu kupunguza gharama za upasuaji kwa kununua vifaa moja kwa moja kutoka viwandani

Prof Makubi.

Mipango mingine ni kuendelea kuwapa mafunzo wataalamu ili kuwaongezea ujuzi ambapo wataamu 10 wanapelekwa kwenye mafunzo kupitia mfuko wa mafunzo wa Mama Samia. 

Aidha kuendelea kujiengea uwezo watumishi wa Hospitali zingine za Kanda na Mikoa ili kupunguza mrundikano wa wagonjwa MOI na kutoa nafuu ya gharama kwa Wananchi.

Kutoa elimu kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ili kupunguza ajali za barabarani na kukabiliana na majeruhi kwa haraka. 

Pia kuimarisha uwajibikaji na usimamizi kwa viongozi na watumishi ndani ya taasisi, kuendelea kushirikiana na MUHAS na MNH. 



 

 

Post a Comment

0 Comments