MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM mkoa wa Dodoma Donald Mejitii amekiri kufurahishwa na utayari wa wananchi ambao ni Wakulima kwa kuwa wabunifu kupitia mazao ya ndani kwa kuongeza mazao mnyororo wa thamani.
Amesema hayo jijini Dodoma Wakati alipokuwa akitembelea mabanda katika sherehe zinazoendelea za maonesho ya Wakulima na wafugaji Nzuguni Dodoma.
Nimefurahishwa kuona mazao yameongezewa thamani kwani huko nyuma tulikuwa tukivuna mavuno kutoka shambani na kupeleka sokoni lakini sasa mambo yamebadikika ambapo tunaona Alizeti mchakato wake unaleta sabuni, mkaa mafuta ya kupikia ni mambo makubwa huku nyuma hayakuwepo
Mejiti
Amesema kupitia awamu ya mikopo ya Halmashauri vikundi vingi vimepata mikopo ya asilimia 4 vijana na akina mama wamewezeshwa ambapo mafanikio kwa vijana na Wanawake ni makubwa.
Hivyo jamii kuanza kutumia bidhaa zinatengenezwa na wajasiriamali tupitia mazao wanayoongezea mnyororo wa thamani
Mejiti
Aidha amesema zipo bidhaa nyingi zinazotokana na kilimo hivyo ni wakati sasa kwa Tanzania kutumia bidhaa hizo kutoka kwa wajasilimali wetu.
0 Comments