MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano
wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) imeandaa kongamano la ajira litakalofanyika
siku Alhamisi tarehe 24 Agosti katika uwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Abdallah Ngodu amesema kuwa katika kongamano hilo
kutakuwa na maonyesho ambayo yamelenga kujenga uelewa juu ya fursa za ufundi stadi zilizopo kwenye mradi wa kukuza
uwezo wa kuajirika [kujiajiri/kuajirika] kwa wahitimu / wanufaika wa kozi
zinazotolewa na Vyuo vya VETA chini ya mradi
wa E4DT
Kupitia kongamano hilo wanafunzi/ wanufaika watakutanishwa na waajiri ili waweze kushirikiana kuhusu taarifa za soko la ajira halikadhalika wahitimu wataonesha umahiri wa ujuzi wao katika bidhaa walizotengneza na miradi yao wanayotekeleza
Ngodu
Aidha ameongeza kuwa wananchi watapata fursa ya kujionea shughuli zinazofanywa na wahitimu/ wanufaika wa mradi wa E4DT pamoja na kupata taarifa juu ya fursa za mafunzo ya vyuo vya VETA nchini.
Hata hivyo utekelezaji wa mradi wa E4DT unahusisha ushiriki wa viwanda ambapo mpaka sasa viwanda na makampuni zaidi ya 20 yamethibitisha kushiriki na kuonesha huduma na bidhaa zao kupitia kongamano hilo.
Tunaamini kuwa makampuni pia yatapata fursa muhimu ya kuthibitishwa kwa uhalisia kuhusu umahiri na ujuzi wa wahitimu / wanufaika wa mafunzo ya ufundi stadi ili wajenge imani na hatimye kuwapa fursa za ajira vijana hao.
0 Comments