KATIBU Mkuu
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi Balozi Aisha
Amour amewataka wafanyakazi wa Bodi ya usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi (AQRB), kufanya kazi kwa kujituma na kuepuka Vitendo vya
Rushwa.
Balozi Amour ametoa kauli hiyo Leo Agosti 29, 2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha tisa cha Baraza la Wafanyakazi wa Bodi ya usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majengo (AQRB).
Kutokuwa na weledi na uadilifu na uwepo wa makundi inapelekea kudorora kwa ufanisi wa utendaji kazi baina yenu kama watumishi wa umma. Na nitangaze rasmi hapa hatutaweza kumvumilia mtumishi yeyote atakayekuwa kikwazo katika utendaji kazi
Balozi Amour.
Katibu Mkuu huyo amesema hakutakuwepo na nafasi ya kumhamisha mtumishi wa umma kisa ameshindikana au kashindwa kutimiza majukumu yake vyema kwa nafasi aliyonayo
Ni vyema kumuondoa kwenye mfumo wa ajira ili wengine wachukue nafasi na kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.
Pia amewapongeza viongozi wa bodi hiyo kwa kufanya kikao hicho ambacho ndani yake kutakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya maadili ya kazi .
Wakati huo huo ameagiza ufuatiliaji wa uwepo wa vitendo vya rushwa baina ya wafanyakazi wa bodi hiyo hasa pale wanapokwenda kupima na kukagua majengo.
Nawaagiza fuatilieni suala la kupokea rushwa baina ya wafanyakazi wenu hasa pale wanapokwenda kufanya vipimo na kukadiria Majengo.
Balozi Amour.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majengi (AQRB) Mbunifu Majengo Edwin John Nnunduma, amesema kuwa bodi hiyo ina watumishi wa kudumu 42 na watumishi wa mikataba 16 ambao wanafanya jumla ya watumishi wa bodi kuwa 58 na kwa mujibu wa muundo mpya wa bodi, IKAMA ya Bodi inatakiwa kuwa na Watumishi 114 hivyo kuna upungufu wa watumishi 56.
"Matarajio
ya utendaji kazi kwa watumishi ni kutoa majibu sahihi na kwa wakati, kuwa
wawazi katika utendaji, kumjali na kumheshimu mteja, matumizi sahihi ya taarifa
za bodi na Serikali, kuzingatia viwango, weledi na maadili ya taaluma,
kuzingatia huduma inayotolewa inaendana na thamani ya fedha zinazotumika, kuwa
tayari kujifunza na kubadilika, na kutoa huduma kwa kutumia teknolojia ya kisasa."
0 Comments