📌RHODA SIMBA
MKUU wa Bodi ya Katani Tanzania (TSB) Saddy Kambona amesema kuwa Katani ya Tanzania ina ubora zaidi wa kutengenezwa sukari kuliko aina ya katani inayozalishwa nchini Mexico.
Kambona ameyasema hayo leo Agosti 16 jijini Dodoma wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TSB kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema baada ya katani ya Tanzania kupimwa ughaibuni ikabainika ina sukari mara dufu kuliko katani inayozalishwa Mexico na hivyo ikatokea wawekezaji ili wajenge kiwanda nchini cha kuzalisha sukari, mpango ambao bado haujafanyika.
Ikumbukwe kuwa zao la Mkonge lina historia ndefu nchini. Ni zao ambalo liliingizwa mchini mwaka 1893 na Mtafiti wa kilimo raia wa Ujerumani anayefahamika kwa jina la Dkt Richard Hindolf ambaye alichukua mbegu za mkonge kutoka Mji wa Yucatan Nchini Mexico.
Nchini Tanzania zao hili lilianzia Wilayani pangani Mkoani Tanga na baadaye kuenea katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro, Arusha na maeneo mengine
Amesema Mkonge ulikuwa unalimwa na wakulima wakubwa pekee waliokuwa wanamiliki mashamba makubwa (Estates/Plantations). Hakukuwa na wakulima wadogo wa Mkonge.
Kadhalika amebainisha kuwa uzalishaji wa Mkonge uliongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia mwaka 1964 Tanzania iliweza kuzalisha takriban Tani 230,000 na kuongoza Duniani kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.
0 Comments