KAIRUKI AWATAKA MAAFISA NA MAWAKALA KUSIMAMIA VYEMA UKUSANYAJI WA MAPATO

 ðŸ“ŒSUZANA ALEX

WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe, Angellah Kairuki amewataka maafisa na mawakala waliopewa dhamana ya kukusanya mapato ya Halmashauri kusimamia ipasavyo eneo la ukusanyaji wa mapato.

Ameyasema hayo Agosti 17, 2023 alipokua akizungumza mbele ya wahasibu na waweka hazina wa halmashauri katika kikao Cha kufunga hesabu za mwaka 2022_2023  ambapo kina siku4 toka kilipoanza .

Ameendelea kwa kusema hakikisheni mnasimamia vyema ili kuondoa mianya ya upotevu wa mapato

Ni imani yangu  mtaendelea kusimamia vyema na hakutakuwa na changamoto.Ni muhimu kuhakikisha tunafunga hoja za ukaguzi pasibaki na hoja hata moja ambayo haijafungwa au kutowekewa maelekezo ipasavyo

Kairuki.

Pia amesema kuwa kama serikali itaendelea kutatua changamoto za kitaaluma na kitaalamu wanazopitia wafanyakazi hao na kutenga bajeti kwaajili ya mafunzo zaidi hatua hiyo itawezesha ongezeko la ukusanyaji   mapato.

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa kamati ya kufunga hesabu George Eston amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuangalia mapitio ya hesabu walizofunga mwaka jana na kuangalia ufungaji wa hesabu za mwaka huu wa fedha katika Halmashauri zote 184 zilizopo nchini.

Hesabu hizi tunategemea kufikia tarehe 31 mwezi wa 8 kila halmashauri iwe imepata hesabu zake draft ya kwanza ambayo tutaiwasilisha kwaajili ya ukaguzi na kuzipitisha kwenye kikao ili tarehe 30 mwezi wa 9 hesabu zetu ziweze kuwasilishwa.

 

Post a Comment

0 Comments