KAIMU Mkurugenzi wa habari na uhusiano
makao makuu ya jeshi, Jeshi la ulinzi la wananchi Tanzania JWTZ Luteni Kanali
Gaudentius G Ilonda amewataka wananchi wanaovaa mavazi yanayofanania
na jeshi au kuelekea kufanana waache na badala yake wayarejeshe
katika kambi ya jeshi,vituo vya polisi au ofisi za serikali vilivyopo karibu
Yao Ili kuepuka usumbufu.
Ameyasema hayo leo, kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dodoma na kueleza kuwa jeshi hilo linatoa siku saba agizo hilo kukamilika.
Tunatoa siku 7 kuanzia Leo mavazi haya ndio iwe mwisho wa kuvaa,kuyatumia ama kuyauza atakayekutwa na mavazi aya atachukuliwa hatua na itakua fundisho Kwa wengine
Ilonda
Aidha ameendelea kwa kusema sheria ya ulinzi wa taifa inakataza, sheria ya taifa na sheria ya kanuni ya adabu zote zinakataza kuvaa mavazi kama combati, t-shirt, kofia, kaptula, magauni, viatu hata mabegi au mishono imeshonwa kwa mtindo kama huo katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 sura 192 sheria namba 24, sheria ya mwaka 1966 marejeo 2002.
0 Comments