KAIMU Mkurugenzi wa habari na uhusiano
makao makuu ya Jeshi JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda ametoa katazo
la uvaaji wa nguo za kijeshi jana wakati akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma
Amesema kuwa mavazi hayo ni pamoja na Kombati (vazi la mabaka mabaka) Makoti, tisheti, suruali, magauni, kofia, viatu mabegi na kaptula zenye rangi zinazofanana au kushonwa katika mitindo ya kijeshi
Ameongeza kwa kusema katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya ulinzi wa taifa (NDA) sura ya 192 Sheria namb 24 ya mwaka 1996 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Aidha ameongeza kwa kusema kifungu cha 178 cha Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 (Penal code) na kifungu cha 6 cha Sheria ya usalama wa taifa vinakataza raia kuvaa sare na mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo
Ndio maana tunatoa siku saba kujisalimisha bila kuchukuliwa hatua ili kuepuka usumbufu na jeshi na ambaye hatayawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya
Ilonda
Hata hivyo amesema zipo baadhi ya taasisi zinazowashonea watumishi wake sare aina hiyo, wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo yao ya biashara
JWTZ linaomba kupitia kwenu kuwafahamisha wananchi kuwa utekelezaji wa majukumuu yake ya msingi na mengineyo tunagemea sana ushirikiano mzuri na wananchi wote pia limeongeza kwa kusema sio hekima kwetu kulumbana kwa namna yoyote ile na baadhi ya wananchi wenye mavazi yaliyokakatazwa
Wapo baadhi ambao kwa kuyatumia mavazi hayo wamekuwa wakitapeli wanachi na wengine kufanya vitendo viovu ambao pia wamekuwa wakidhaniwa kuwa ni wanajeshi
Ilonda
0 Comments