MKUU
wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,
anawataarifu vijana wote wa Tanzania Bara na visiwani nafasi ya kujiunga na
mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka 2023.
Taarifa hii imetolewa Leo Agosti, 25 2023 na Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 25,2023 Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya MKUU wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele
Usahili wa vijana hao wa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 28 Agosti, 2023 kwa mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani vijana watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti makambini kuanziaa tarehe 26 Septemba hadi tarehe 29 Septemba 2023.
Vijana watakao ripoti makambini wanatakiwa kuripoti na vifaa ambavyo ni bukta ya rangi ' Dark blue' yenye mpira kiunoni (lastic) iwe na mfuko mmoja nyuma urefu unaoishia magotini isiyo na zipu kwa vijana wa kike iwe na mpira kiunoni na kwenye pindo za miguu, Raba za michezo rangi ya kijani au blue , shuka mbili za kulalia rangi ya blue bahari , soksi ndefu nyeusi nguo za kuzuia baridi kwa wale watakaochaguliwa kwenye mikoa ya baridi
Mabena
Utaratibu wa kuomba na kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na Ofisi za wakuu wa Mikoa na wilaya ambako muombaji anaishi.
Sifa za muombaji lazima awe raia wa Tanzania wenye elimu ya darasa la Saba awe na umri kuanzia miaka 16 hadi 18 waliomaliza elimu ya msingi kuanzia mwaka 2020, 2021,2022 awe na cheti halisi cha kumaliza elimu ya msingi na kwa kwa wale wenye elimu ya kidato cha nne umri usizidi miaka 20 awe amemaliza elimu ya sekondari kuanzia 2020, 2021 na 2022 awe na cheti halisi cha kumaliza elimu ya sekondari ( leaving certificate) na cheti halisi cha matokeo ( academic certificate) na awe na ufaufu wa daraja la kwanza hadi daraja la nne, kijana mwenye daraja la nne awe na ufaufu kuanziaa 26 hadi 32 na kidato cha sita umri usizidi miaka 25 awe amemaliza elimu ya sekondari kuanziaa 2020, 2021, na 2022.
Pia kwa elimu ya stashahada umri usizidi miaka 25 awe na cheti cha sekondari na chuo, awe na akili timamu asiwe na michoro yeyote ( tattoo), awe na tabia na nidhamu nzuri hajawahi kupata hatia yeyote mahakamani wala kufungwa, asiwe ametumika jeshi la polisi, magereza, chuo Cha mafunzo au kikosi maalumu cha kuzuia magendo au kuajiriwa katika idara yeyote selikarini, asiwe amejihusisha na madawa ya kulevya bangi na yanayofanana na hayo
Mabena
Kijana atakayepatikana na nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na taratibu zilizopo.
Aidha jeshi la kujenga Taifa linapenda kuwataarifu vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira pia halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama .
Mkuu wa (JKT ) Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa ya kujiunga na vijana wenzao ili kujenga uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasio ya kiserikali.
0 Comments