MKURUGENZI wa Tume ya ushindani Tanzania (FCC) Willam Erio amesema kwa mwaka 2022/2023 imefanya mapambano dhidi ya nidhaa bandia ambapo katika kaguzi zake kwenye bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu (ICDs) asilimia 3.4% ya jumla ya makasha (containers) yaliyokaguliwa yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Bilioni 20.8 yalikutwa na bidhaa zilizokiuka sheria ya alama za bidhaa .
Amesema hayo leo Agosti 2 jijini Dodoma na wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
Erio Amefanunua kuwa Kaguzi za kushtukiza (Dawn Raids) zilizofanyika kwenye bidhaa zenye thamani ya Shilingi Billioni 4.7 zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa zilikamatwa na hatua stahiki zilichukuliwa, na kuongeza kuwa Kaguzi hizo zilifanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Songwe, Kilimanjaro, Pwani, Mwanza, Arusha, Katavi na Mbeya.
FCC imefanya uharibifu wa bidhaa bandia zilizokamatwa katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma. Bidhaa zilizoharibiwa ni pamoja na wino wa printa katoni 432 na kilo 1,302 za vifungashio
Erio.
Mbali na hayo tume hiyo imepokea malalamiko 58 ya watumiaji wa bidhaa na huduma zinazohusu mikataba inayoandaliwa na upande mmoja (1), usalama wa bidhaa, upotoshaji katika bidhaa, huduma za kifedha na huduma za Bima.
Pia Malalamiko 21 yaliyohusu masharti ya mikataba inayoandaliwa upande mmoja (1) yalipatiwa ufumbuzi, pia Malalamiko yaliyohusu upotoshaji wa bidhaa yalipatiwa ufumbuzi na Malalamiko 13 yaliyohusu huduma za fedha, usalama wa bidhaa na huduma na Bima ambayo yalihamishiwa katika Mamlaka sahihi ambazo ni TBS, BOT na Jeshi la Polisi.
Malalamiko 19 yako katika hatua mbalimbali za kupatiwa ufumbuzi, FCC imesajili Mikataba 77 iliyoandaliwa na upande mmoja (Standard Form Consumer Contracts) kutoka katika Sekta mbalimbali, Lengo la kusajili mikataba hiyo ni pamoja na kuondoa masharti kandamizi, urahisi wa kueleweka kwa mikataba kwa kutumia lugha rahisi na kuhakikisha mikataba hiyo inazingatia misingi ya ulinzi wa mlaji
Erio.
Akizungumzia mafanikio ya tume hiyo Katika Sekta ya Mawasiliano FCC Erio amesema iliidhinisha jumla ya kampuni 26 zilizonunuliwa na wawekezaji mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2020 na 2023 kwa thamani ya Shilingi Bilioni 653.
Pamoja na hayo Katika mwaka wa fedha 2023/24 FCC imepanga Kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Uendeshaji wa Shughuli za Tume ya Ushindani (FCC – MIS) ambapo Mfumo huu utaongeza ufanisi wa FCC kwa kusogeza huduma kwa wateja.
Tume ya Ushindani (FCC) ni Taasisi ya Umma, iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Ushindani Na. 8 ya mwaka 2003 (FCA), kwa madhumuni ya kukuza na kulinda ushindani katika biashara na kumlinda mtumiaji dhidi ya mienendo dhaifu na kandamizi katika uchumi wa soko.
0 Comments