MENEJA wa Kanda ya kati wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA Hawa Sahani amewataka wananchi na wadau wote kufika katika banda lao ili kuweza kupata elimu juu ya kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja huyo amesema EWURA imekuwa ikisimimia huduma katika Sekta ya Nishati, Mafuta ,Gesi asilia Umeme na Maji.
Aidha amesema Ewura imekuwa ikitoa leseni na kazi kubwa na Msingi ni kusimamia hizo leseni ili Wananchi wote waweze kupata huduma katika ubora zaidi na kuongeza ufanisi katika Mamlaka zote wanazozisimamia kama EWURA.
Aidha Meneja huyo ametoa wito kwa wakazi na wananchi wote kufika ili kuweza kupatiwa ufafanuzi na kujibiwa maswali yote yanayowatatiza au kujiuliza.
Kumekuwa na maswali mengi kwa Wananchi juu ya shughuli zinazofanywa na Mamlaka yetu hivyo ili kuweza kujibiwa maswali yote karibuni katika Banda letu kujibiwa maswali yenu
Hawa
Maonesho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni Msingi imara wa Mifumo endelevu ya Chakula"
Maonyesho ya Wakulima na wafugaji Kanda ya Kati yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya Nzuguni nanenane Dodoma.
0 Comments