📌 AISHA SULEYAM
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wakulima ili kuzalisha mazao kwawingi kwani ndiyo uti wa mgongo.
Mh Senyamule ameseyasema leo Agosti 8, 2023 Jiji la Dodoma wakati akihitimisha maenesho ya siku ya wakulima na wafugaji (Nane nane).
Amesema kila halmashauri nchini itapata visima 150 na hivyo kwa upande wao kama mkoa wako tayari kupokea visima hivyo ili kuweza kuwanufaisha wakulima.alisem Senyamule"
Dodoma tumedhamiria kukifanya kilimo kweli kuwa uti wa mgongo kama Dkt. Samia alivyo ifanya Tanzania kuwa hadhi ya chakula
Senyamule.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Selukamba amesema kuwa pato la mkoa huo linategemea kilimo kwa asilimia kubwa.
Aidha ameongeza kuwa mategemeo yao ni kwamba wakulima elimu waliyoipata itaenda kuwaongezea tija na hivyo kama mikoa miwili ya Singida na Dodoma inayolima alizeti kama zao la mkakati wanategemea kupata faida kubwa na kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika mikoa hiyo.
"Ni vyema Wizara ya mambo ya ndani itangaze haya maadhimisho kimaifa ili wakulima kuweza kupata fursa za kupata masoko zaidi nje ya nchi,"amesema Selukamba.
0 Comments