MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule
amesema kuwa Dodoma kwasasa inajenga miundo mbinu bora kwenye sekta mbalimbali
ambazo ni sekta ya elimu, ujenzi pamoja na afya.
Ameyasema hayo leo mbele ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa jengo la kitega uchumi (Safina house) Jijini Dodoma dayosis ya Central Tanganyika lililozinduliwa na Rais Mh Samia Suluhu Hassan
Idadi ya wanafunzi kidato cha tano sasa imeongezeka hivyo kwasasa tunajenga shule mpya kumi kuanzia msingi mpaka kidato cha nne
Senyamule.
Naye Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Tanga Mhashamu Maimbo Mndolwa amesema Kanisa la Anglikana limekua likishirikiana na serikali kwa ukaribu pia amewashauri viongozi kufanya kazi vyema na kutokuogopa maneno ya watu.
Palipo na kazi yenye nguvu maneno lazima yasemwe, viongozi msikatishwe tamaa na maneno ya watu
Mndolwa.
Dayosisi ya Central Tanganyika ilianzishwa mwaka 1927 kutoka Mombasa kwasasa Tanzania nzima ina jumla ya dayosisi 20.
0 Comments