DKT. IBENZI ATAJA SABABU WANAWAKE KUPENDA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

IMEBAINISHWA kuwa  wanawake wengi kwa sasa  hukwepa maumivu ya uchungu wakati wa kujifungua na kuamua kuomba kujifungua kwa oparesheni njia ambayo imeonekana bora kutokana na uwekezaji wa vifaa bora na vya kisasa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita .

Hayo yamesemwa leo Agosti 9 jijini Dodoma na Mganga Mkuu mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt Ernest Ibenzi  wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya hospital ya Mkoa wa Dodoma na mwelekeo wa utekelezaji katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Zamani wajawazito walikuwa wanajifungua kwa operation halafu wanakandwa maji ya moto na hali hiyo ilikuwa inawafanya vidonda kuharibika, vifo kwa sasa vya mama wajawazito vimepungua kwani mpaka sasa tunaweza kukaa miezi minne bila ya kuwa na vidonda vitokanavyo na upasuaji

Ibenzi

Amesema Hospitali imefanikiwa kununua vifaa tiba vya kisasa ikiwemo; CT- Scan, X- Ray mashine 3 za kisasa zaidi kutoka mashine 1, mashine za Ultrasound 4, mashine za kisasa za maabara na vitendanishi, tunafanya vipimo 136 vinavyosaidia wananchi kutambua changamoto mbalimbali za afya zao.

Hospitali ina vyumba 12 vya kufanyia upasuaji (oparesheni) na kwa siku takribani wagonjwa 70 wanafanyiwa oparesheni, Hospitali ilikuwa na ufinyu wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje na dharura ambalo lilikuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 4 tu wa dharura kwa wakati mmoja

 

 

Post a Comment

0 Comments