MKURUGENZI
Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt . Alphonce Chandika ametaja
gharama za kupandikizwa uume kuwa ni kati ya Shilingi milioni 6 hadi Shilingi milioni 10.
Ameyasema hayo leo Agosti 1 jijini dodoma wakati akielezea vipaumbele vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24 Dkt Chandika amesema huduma hiyo imeanzishwa baada ya kubaini kuwa kuna changamoto kubwa ambayo imewafanya waganga wa kienyeji kupita mitaani na dawa zinazodaiwa kutibu tatizo hilo.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya wanaume wawili waliofanyiwa upandikizwaji amesema habari njema kutoka kwa wanaume hao, mambo yamekuwa mazuri na kwamba hivi sasa wako katika mkakati wa kupanua wigo wa huduma ili kuifanya ipatikane kwa kila anayehitaji
Aidha, Dk Chandika amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 wametengewa Sh bilioni 64.52 na kwamba Shilingi bilioni 18.62 zitakwenda katika miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.
Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la saratani, jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wazima na kituo cha upandikizi wa figo.
0 Comments