CWT KUJIANDAA MAPEMA MASHINDANO YA SATO MSIMU UJAO

 ðŸ“ŒSUZANA ALEX

MAKAMU wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Suleiman Komba amesema wanatarajia kuanza maandalizi mapema kuiandaa Timu ya chama cha walimu kuelekea mashindano ya Southern African Teachers Organization (SATO) msimu ujao.

Suleiman ameyasema hayo Jijini Dodoma  wakati akipokea Timu ya Chama hicho iliyotokea Gaborone nchini Botswana kwenye mashindano ya kimataifa ya walimu yaliyozikutanisha nchi 11 za kusini mwa Afrika

Nia  yetu ni kuongeza wigo  kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inatoa uwakilishi  na idadi kubwa ya wachezaji. Mwaka huu tumeenda na idadi ndogo hivyo tunajipanga mwakani kwenda na idadi kubwa ya wachezaji ili tupate uwakilishi mkubwa kwenye kila mchezo na kupunguza uchovu wa wachezaji unaotokana na kushiriki michezo mingi hivyo niwaombe walimu muanze kuziandaa Timu zenu mapema

Mpango wetu ni kuanzisha mashindano  mbalimbali kila Mkoa  yatakayotuwezesha kupata wachezaji walio bora kwenye kila mchezo mashindano haya ya mikoa  yatatufanya tuwe bora kwenye mashindano yajayo

Kwa upande wake Mratibu wa mashindano Chama cha Walimu (CWT) Prosper Rubuva  amesema moja ya changamoto walizozipitia kwenye mashindano ya SATO  msimu huu ni pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wachezaji kitu kilichopelekea wachezaji wao kijirudia kwenye baadhi ya michezo.

Tumeenda walimu wachache kwenye mashindano, uchache wetu unatupa shida kubwa katika michezo mingine maana mchezaji mmoja anatakiwa acheze mchezo zaidi ya mmoja lakini pamoja na uchache wetu tumeendelea kufanya vizuri

 Rubuva

Timu ya Walimu imewasili Jijini Dodoma ikitokea Gaborone Botswana ambapo imechukua nafasi ya nne kwa washindi wa jumla

Post a Comment

0 Comments