TUME ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),
imesema kuwa itaendelea kushirikiana na mabaraza ya kikanda na kimataifa
kuhakikisha inashiriki kutafuta fursa za wabunifu ambazo zitaendelea kuleta
fedha kupitia tume hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma Agosti 25, mwaka 2023.
Vipaumbele vya Tume kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni kusimamia miradi inayoendelea ukiwemo wa kigoda cha utafiti SUA na NM-AIST ambao ni mradi wa miaka mitano, wenye thamani ya takribani billion 5
Nungu
Aidha ameendelea kwa kusema Tume hiyo inafanya zoezi la ufadhili wa pamoja wa miradi ya utafiti wa mabaraza ya utafiti duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza kuonekana kwa watafiti wetu na kuitangaza nchi yetu katika nyanja hii ya utafiti pamoja na kukamilisha mchakato na kutoa fedha kwa maandiko mawili kwa kutoa mrejesho kwa walioshiriki lakini wakakosa na kuwatembelea walioshinda.
Kuwasaidia DTBi kukamilisha karakana iliyopo SIDO vingunguti ili kuzalisha mita za maji Kwa mikoa 15 iliyobaki, kusimamia kongamano la bunifu mpya ikiwemo ya Mafia (Nazi) na Kigoma (mawese) na kufanya kazi na kumbi za wabunifu na wadau wengine kuhakikisha mazingira wezeshi yanaimalika zaidi
Nungu.
Tume hiyo haifanyi utafiti bali inaratibu na ni Taasisi ya umma ambayo ni mshauri Mkuu wa serikali.
0 Comments