𝗥𝗖 𝗠𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗔𝗜𝗣𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗔 𝗲-𝗚𝗔 𝗞𝗨𝗛𝗔𝗞𝗜𝗞𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗧𝗔𝗔𝗦𝗜𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗨𝗠𝗠𝗔 𝗭𝗜𝗡𝗔𝗧𝗢𝗔 𝗛𝗨𝗗𝗨𝗠𝗔 𝗞𝗜𝗗𝗜𝗚𝗜𝗧𝗔𝗟𝗜

 📌MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa jitihada kubwa inazofanya za kuhakikisha Taasisi za umma zinatoa huduma kidigitali.

Mtaka ametoa pongezi hizo leo, alipotembelea katika banda la e-GA kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya. 

Mimi niwapongeze sana, mmekuwa mkifanya kazi nzuri ya kuhakikisha Serikali inatoa huduma zake kwa urahisi kupitia mifumo ya TEHAMA, rai yangu endeleeni kuja na bunifu mbalimbali lakini pia mhakikishe Taasisi zinaungana

Ameongeza kuwa, kwa muda mrefu  Mamlaka ya Serikali Mtandao imekuwa ikija na bunifu za mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayorahisisha utendaji kazi na kufanya huduma za Serikali zipatikane kwa urahisi.

Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Serikali Mtandao, Rainer Budodi alisema kuwa, Mamlaka inatoa elimu kwa wananchi wanaofika katika banda hilo ili waweze kufahamu na kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA iliyotengenezwa na Mamlaka.  

Amesema kuwa,  baadhi ya mifumo ya TEHAMA ambayo e-GA inatoa elimu kwa wananchi wanaotembelea katika banda hilo ni pamoja na Mfumo wa e-Mrejesho ambao unawawezssha wananchi kuwasiliana na serikali kidijitali, Mfumo wa ubadilishanaji taarifa serikalini (GoVESB), Mfumo wa huduma za serikali kupitia simu za mkononi (MGOV) pamoja na  Mfumo wa ukusanyaji wa data na takwimu (e-Dodoso)

Budodi alimshukuru kiongozi huyo kutembelea banda la Mamlaka, na kuwasihi viongozi na wananchi wengine kutembelea banda hilo ili kujionea bunifu mbalimbali za mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa na vijana wa kitanzania kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Mamlaka ya Serikali Mtandao e-GA kwa mwaka huu 2023 inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya wiki ya wakulima (nanenane) ambayo kwa mwaka huu maonyesho hayo kitaifa yanafanyika jijini Mbeya.


 

Post a Comment

0 Comments