BILIONI 858 YAIDHINISHWA KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA ZA WILAYA

 ðŸ“ŒMWANDISHI WETU

DODOMA Jumla ya Sh. bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za wilaya. Kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 710.31 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mhandisi Victor Seff amesema, takwimu zinaonesha kuwa asilimia 71.48 ya mtandao wa barabara za wilaya ni za udongo, hali inayo sababisha kutopitika kwa urahisi wakati wa mvua. 

Changamoto hiyo inadhoofisha ukuaji wa sekta ya kilimo, kupanda kwa gharaza za usafirishaji, na pia kutofikika kwa huduma za kijamii na kiuchumi kwa maana ya shule, vituo vya afya, masoko pamoja na ajira.

Mhandisi Seff. 

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, jumla ya barabara zenye urefu wa km 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo, km 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, km 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa pamoja na mifereji ya mvua km 70.

 

Post a Comment

0 Comments