WANANCHI WATAKIWA KUFIKA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 60 YA JKT VIWANJA VYA SUMA JKT

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WANANCHI wote hasa waishio katika Jiji la Dodoma wametakiwa kufika kwenye maonesha ya wiki ya kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kuweza kujifunza na kunufaika na elimu inayotolewa na Jeshi hilo.

Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Suma JKT mjini Dodoma kuanzia Julai 1 Hadi 9 ambapo shughuli mbalimbali zinaendelea katika maonesho hayo .

Makamu wa Rais Dkt,Philip Mpango ameyasema hayo jijini Dodoma kwenye ufunguzi ya wiki ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa  (JKT) .

Dkt, Mpango amesema  kufuatia maonesho hayo ya JKT viongozi wote hasa wakuu wa mikoa hawanabudi kufika na kujifunza elimu yote inayotolewa  .

Pia amewataka Wananchi mikoa yote kujitokeza kwawingi katika wiki ya maonesho kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa ili kupata elimu na ufahamu juu ya shughuli za JKT

Aidha Dkt Mpango ametoa rai kwa JKT kupitia maadhimisho hayo kuendelea kujitanua kwa kujitangaza na kuendeleza ushirikiano baina  yao na Wananchi .

Kupitia maonesho haya na uwepo wa  wadau wengine ni wazi kuwa itaifanya JKT kujipima katika ushindani wa utengenezaji wa bidhaa

Katika  kutekeleza dhima yenu ya kuwafundisha vijana ujuzi, na ukakamavu muendelee kutilia mkazo katika suala zima la ulinzi wa Mazingira ni lazima kuwekeza nguvu kwa vijana juu ya kutunza mazingira na ongezeni bidii kwenye kupanda miti pia kufanya usafi kwenye kambi zetu

Dkt Mpango

Hata hivyo ameitaka JKT kuongeza matumizi ya Teknologia katika kazi zao kwani  zama za sasa siyo zama za kutumia misuli na badala yake  wawatambue wataalam wenye ubunifu kwa kuwapatia tuzo.

Pia niwaombe ongezeni msukumo katika kuibua vipaji kwenye michezo na nitoe pongezi kwa timu zetu za Jeshi ambazo zinafanya vizuri katika maeneo mbalimbali.
 

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa JKT limetimiza majukumu yake ya Msingi katika kuleta Umoja wa Vijana.

Aidha JKT inaendeleza shughuli za uzalishaji mali kupitia Shirika la SUMA JKT Kwa kutoa huduma mbalimbali, SUMAJKT toka kuanzishwa kwake limefanikiwa kushiriki katika kuongeza ajira hapa nchini.

Tunapoelekea kilele cha maadhimisho ya JKT, JKT imejipanga kutoa elimu ya kilimo kwa Wananchi watakaotembelea maeneo ya maonesho halidhalika kutakuwepo na wanyama ambao ni rafiki katika maeneo haya

Mabele 

Aidha ameongeza kuwa kutakuwepo na mabonanza ya mpira wa miguu, mpira wa pete pia kutakuwepo na shughuli mbalimbali kama kuwatembelea watu wenye mahitaji muhimu na kuchangia damu.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa amesema kuwa kupitia kampuni ya SUMA JKT imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Ikulu ya Chamwino.

Pia Wizara itaendelea kuijengea uwezo JKT katika kutimiza majukumu yake kupitia kampuni ya SUMA JKT

 

Post a Comment

0 Comments