TFRA KUHIMIZA UZALISHAJI MBOLEA BORA NCHINI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema inahakikisha inaongeza na kuimarisha upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa mbolea bora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA) Dkt.Stephan Ngailo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na muelekeo kwa mwaka 2023/24.

Amesema kuwa dhima ya TFRA ni kuhakikisha upatikanaji, ufikiwaji, uwezo wa kumudu na ubora wa mbolea na visaidizi vyake kwa wakulima wote kwa njia ya udhibiti wa shughuli za mbolea kwaajili ya uendelevu wa uzalishaji wenye tija katika kilimo.

TFRA inashirikiana na sekta binafsi kuimarisha upatikanaji wa mbolea bora inayozalishwa na kuingizwa nchini na kupanua mtandao wa usambazaji na kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji

Sambamba na kuratibu na kusimamia utekelezaji wa utoaji wa mbolea ya ruzuku, Kuratibu upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini (tani 850,000), Kuendelea kudhibiti ubora wa mbolea, Kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea nchini, Kushirikiana na wadau kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea, Uimarishaji wa maabara ya uchambuzi wa mbolea

Kadhalika ameeleza kuwa kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

Lengo ama dhamira ya serikali ilikuwa ni pamoja na kupunguza gharama ya mbolea, kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Kilimo, Sheria ya Mbolea Namba 9 ya Mwaka 2009 (Fertilizer Act, 2009) na kanuni zake za Mwaka 2011,TFRA ilianza kutekeleza majukumu yake mnamo Agosti 2012.

 


Post a Comment

0 Comments