KAMISHINA wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) William Mwakilema amesema Shirika limeanzisha programu maalum ya kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia kiasi cha shilingi Milioni 5.
Aidha amesema Programu hiyo inakuja kufuatia baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Juniour, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.
Kamishina Mwakilema ameyasema hayo leo Julai 24 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.
Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako
Amesema bodi ya menejimenti ya TANAPA imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.
Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.
Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.
Ameelezea asili ya Bob junior (simba aliyepewa jina la bob Junior), Kamishna Mwakilema amesema jina hilo alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo wakamlinganisha na Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta zake nyingi, ukubwa na kivutio kwa watalii.
Bahati mbaya jina hilo halikutambulika hadi alipokufa akaanza kuvuma kuwa bob junior amekufa
0 Comments