RC SENYAMULE AZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI DODOMA.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,.Rosemary Senyamule amezindua Mpango Mkakati wa kushughulikia na kutatua migogoro ya ardhi kwa jiji la Dodoma huku  akiwaasa wananchi na wakazi wa Dodoma kuacha kudanganya maeneo ya makazi ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo  jijini Dodoma Senyamule amesema  jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko la wananchi hivyo kufuatia ongezeko hilo limepelekea matumizi ya ardhi kuwa ni mengi na mengine kuwa ya kiholela bila mpangilio ambapo kwa kutatua changamoto hiyo Mkoa wa Dodoma kupitia Mkuu wa mkoa imeandaa timu kwa ajili ya kutatua na kumaliza migogoro.

Kuna changamoto mbalimbali zinazochangia migogoro hii kushindwa kuisha kutokana na uchache wa vifaa vya tehama, ukosefu wa huduma bora kwa wananchi, eneo la jiji kuwa dogo, lugha mbaya kwa wananchi zinazotolewa na watumishi wa jiji, kipandikizi yaani kupandikiza zaidi ya kiwanja kimoja kupewa watu tofauti pamoja na wananchi kupuuza jumbe za simu

Senyamule.

Aidha ameongeza kuwa jambo hilo litafanyika ndani ya miezi 6 yaani Julai hadi Disemba ambapo kutafanyika uhakiki wa maeneo ambayo yana malalamiko ambapo wahusika wanavamia maeneo ambayo sio ya kwao pamoja na kurekebisha mifumo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amesema kuwa mpango huo utaweza kuwasaidia kutambua mapungufu gani ya ndani na madhaifu ya nje ili kuishi matarajio ya kiongozi wa kitaifa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha jiji la Dodoma linapagwa vizuri ili kuendana na hadhi ya makao makuu ya nchi.

Amesema ni matumaini yake kwamba elimu ya kutosha itatolewa kwa kamati ili kuhakikisha wanakuwa na uelewa huku akisisitiza maeneo ya wazi kupewa watu sahihi ili kuhakikisha wanajenga vitu vyenye manufaa kwa wananchi.

Aidha ametoa rai kwa watumishi wa ardhi kuhudumia wateja vizuri kwa kutoa kauli nzuri kwa wateja pamoja na kuheshimu watu.



Post a Comment

0 Comments