RAIS SAMIA AONGOZA HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA TANZANIA & EU

📌 JASMINE SHAMWEPU

RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan ameongoza hafla ya utiaji saini mikataba mitatu Kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya iliyolenga kuongeza ufanisi kwenye uchumi wa Buluu, kuwezesha mifumo ya kiuchumi na sekta binafsi na kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo mbili 

 

Mikataba hiyo yenye thamani ya shilingi bilioni mia nne sitini na nane imesainiwa sambamba na utoaji wa shilingi bilioni mia moja na arobaini kutoka umoja huo kwa ajili ya kusaidia bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2023/24 huku Rais akiahidi fedha kutumika kama zilivyokusudiwa.

 

Mpaka sasa, Tanzania imeshapokea takriban Euro milioni 2.3 ambayo ni sawa na shilingi trilioni 5.9 kama msaada pamoja na fedha nyingi za mikopo ikiwa ni mikopo ya makubaliano na sio mikopo ya kibiashara kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.

 

Mikataba hiyo ilisainiwa mbele ya Rais Dkt Samia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dk Natu El Mamry Mwamba kwa niaba ya serikali ya Tanzania na balozi wa umoja wa ulaya Manifredo Fanti .

 

Amesema Msaada huu umekuwa chombo cha kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Kimkakati nchini Tanzania, miradi ya maendeleo nchini inatekelezwa kwa njia ya "CPA" ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaichukulia kwa uzito mkubwa.

 

Aidha Rais samia akatumia jukwaa hili kueleza namna ambavyo fedha hizo zitasaidia katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya nchi 

 

Fedha hizi zitasaidia sana katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuandaa sera kwenye sekta ndogo ya uchumi na kijamii, maendeleo ya barabara usafiri wa anga, uboreshaji wa sekta za nishati na kilimo , mazingira na mabadiliko ya tabia nchi 

SAMIA BBT Tanzania inatekeleza mradi wa jenga kesho bora kwa vijana na wanawake katika kilimo hivyo tunategemea Benki ya maendeleo ya kilimo na benki ya uwekezaji Tanzania kufadhili vijana na wanawake wanaojihusisha na mradi huu

Dkt Samia

 

Ombi langu kwa unyeyekevu ni kuomba Umoja wa Ulaya kuzingatia kuziongeza Benki hizi mbili katika mipango ya utoaji mikopo ambayo imenufaisha baadhi ya benki nyingine ambapo 
UE inalenga kuionyesha kwamba hatupo tu katika ushirika wa kiuchumi bali pia ni washirika wa kuleta usawa utulivu na kesho bora kwa watu wa tanzania

Hata hivyo Rais Dkt Samia ametoa ombi kwa umoja huo kusaidia mradi wa kilimo wa jenga kesho bora kwa vijana na wanawake kwa kuzifadhili benki ya maendeleo ya kilimo na benki ya uwekezaji Tanzania ambazo zinatoa mikopo kwa wanufaika wa mradi huo ili kuuongezea tija 

 

Wakizungumza baada ya hafla hiyo Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa TAMISEMI wamesema fedha hizo zitasaidia  kutengeneza ajira, kupunguza umasikini na kukuza uchumi

 

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema juhudi za Rais Samia ndio zimewezesha  nchi kufanya kazi pamoja na Wadau wa Maendeleo katika mchakato wa kujiletea maendeleo.

 

Waziri wa Fedha amesema Tanzania na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya wana mahusiano ya zaidi ya miaka 48, katika miaka yote hiyo Umoja huo umeendelea kuwa karibu na Tanzania. Chini ya uongozi wako, tumeshuhudia mafanikio makubwa ikiwemo kusainiwa kwa Mpango mpya wa ushirikiano kwa Tanzania utakaodumu katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021-2027.

 

Katika uongozi wako, tumeimarisha uhusiano wetu na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya ambayo imekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika miradi yetu ya maendeleo ikiwemo malipo ya Dola za Marekani milioni 12 kati ya Dola za Marekani milioni 67.87 kwa ajili ya kuboresha Viwanja vya Ndege vya Mikoa ikiwemo Kigoma, Tabora, Bukoba, Sumbawanga na Shinyanga

 

 

Post a Comment

0 Comments