RAIS DK SAMIA KUHUTUBIA MKUTANO MKUBWA WA USALAMA WA CHAKULA AFRIKA

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wafanyabiashara wa sekta ya Uvuvi na Mifugo watakaoshiriki mkutano wa Jukwaa la chakula Afrika 2023 ambao kwa mara ya pili unafanyika hapa nchini, kuhakikisha wanaondoka na faida kutoka kwa washiriki wa nchi zingine ambao watakuja kujifunza shughuli hizo.

Waziri Ulega ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau watakaoshiriki mkutano wa Jukwaa la chakula Afrika ambapo amewataka washiriki hao kuwa wepesi kuchangamkia fursa yoyote itakayoonekana ili kuweza kuongeza mitaji.

Wadau niwasihi msizubae mkakosa fursa mbalimbali zitakazoonekana siku ya mkutano ili muongeze ujuzi kwa njia ya tehama na teknolojia mpya ambazo sisi bado hatujazifikia na itawasaidia na nyie kujulikana na kujipatia wateja kutoka mataifa mengine nje ya Tanzania

Na ndio dhumuni kubwa la mkutano huo ambao Rais wa Tanzania alijitoa kimasomaso kuomba ufanyike Tanzania awamu hii kwakua tuko tayari kuundaa hata kama tunakutana na changamoto tujitahidi kuzitatua na kusonga mbele zaidi ili kama nchi tufanikiwe.

Ulega

Nao wadau wa Mifugo na Uvuvi Tanzania wamesema bado wanakutana na changamoto za masoko ya mazao yao hasa kutoka nchi za nje kutokana na kukosa fursa mbalimbali za kimataifa hali inayowaweka mbali na wawekezaji katika sekta ya kifedha ambazo kama wakikutana nazo wanaweza kuongeza mitaji yao na kuongeza tija ya mazao yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania Angelina Ngalula ameitaja Sekta ya Uvuvi na Mifugo ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuzalisha kwa tija ili nchi ionekana kimataifa katika sekta mbalimbali ikiwemo hiyo ambayo inafanywa na watu wengi huku akiwataka washiriki wajue wanataka nini katika mkutano huo na kama bado wajipange kujua manufaa watakayotokana nayo katika mkutano huo.

Nae Mwakilishi Mkazi ,Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo na Muwakilishi wa Benki ya Dunia kwa pamoja wameipongeza Tanzania na kuahidi kuendelea kutoa ushirikino wa hali na mali katika kuifanya Tanzania inaongeza ushindani kibiashara kimataifa ili kuhakikisha malengo waliyoyaweka wanayafikiwa na kuondoa umaskini Tanzania kwa watu kufanya shughuli za kujiajiri wenyewe katika sekta mbalimbali zikiwemo Mifugo na Uvuvi.  

Kwa upande wake muwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda na Bisahara Dk. Joseph Mhagama amewashauri wasimamizi wa sekta ya Kilimo na Uvuvi kuhakikisha wanawasaidia watu wenye nia ya kufanya shughuli hiyo ambayo inalenga kuongeza ajira na vipato kwa makundi ya wanawake na vijana na kupunguza hali ya utegemezi.




 

Post a Comment

0 Comments