MAMLAKA ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma Nchini (PPRA) pamoja na Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wameingia Mkataba wa Hati
ya makubaliano ya mapambano dhidi ya
rushwa katika suala zima la manunuzi ya Umma yenye lengo
la kuzingatia Sheria ili kuondokana na rushwa katika ununuzi wa Umma na kutoa
onyo kwa Taasisi yeyote itakayokiuka sheria za manunuzi
itawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza
Jijini Dodoma wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mtendaji Mkuu
wa Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma Nchini PPRA, Eliakim
Maswi amesema kuwa kama Mamlaka itazingatia kuendelea
kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uaminifu katika kuzingatia suala la
sheria ya manunuzi pamoja na matumizi mazuri ya fedha za umma kwa manufaa ya
Taifa.
Maswi
ameeleza kuwa Makubaliano hayo ni muendelezo wa Ushirikiano
wa Kitaasisi wenye lengo la kuondoa rushwa katika michakato ya ununuzi
wa Umma Nchini ambapo wameamua kuongeza wigo wa ushirikiano kwa
kuongeza juhudi katika mapambano dhidi ya rushwa.
Mtendaji Mkuu
huyo amebainisha kuwa Mwaka 2010 PPRA na TAKUKURU wailiingia kwa mara ya
kwanza Makubaliano ya Ushirikiano katika kupambana na
rushwa katika Manunuzi ya Umma ambapo TAKUKURU ilipewa jukumu la kufanyia
kazi taarifa zinazotolewa na PPRA ya viashiria vya
Rushwa ambapo ni moja ya hatua katika utekelezaji wa mpango
wa mapambano dhidi ya rushwa na hivyo kuamua kukubaliana kuhuisha
ushirikiano huo kwa kuongeza wigo wa mashirikiano hayo kwani kwenye ununuzi wa
umma ndio kwenye rushwa kubwa hivyo wanahitaji TAKUKURU ambao wana utaalam
kuhusu rushwa kuwasidia katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa kifungu cha nane cha Sheria ya Manunuzi sura ya 410 PPRA wamekasimiwa jukumu la kuhakikisha wanausimamia Thamani ya Fedha za Umma katika suala zima la fedha katika manunuzi kwa kuzingatia haki, ushindani uwajibikaji wa fedha za umma ili kuhakikisha kuna ufanisi katika Sheria za Umma kwa kuweka viwango vya ununuzi ambapo wameweka mfumo mpya wa Nest ambao utawasaidia katika kutekeleza suala zima la manunuzi kwa ufanisi mkubwa.
Amesema
kuwa kutokana na kuona utaalam wa TAKUKURU katika uchunguzi dhidi ya rushwa
tukaamua kuona umuhimu wa kuingia makubaliano hayo pamoja na ukiukwaji wa
sheria wenye jinai katika suala zima la manunuzi ya umma.
0 Comments