PPRA KUENDELEA KUZIFUNGIA KAMPUNI ZITAKAZOKIUKA SHERIA NA TARATIBU ZA MANUNUZI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma   (PPRA) imezifungia  baadhi ya kampuni  kwa kukiuka sheria na kwenda kinyume na utaratibu wa sheria za ununuzi wa Umma.

Akizungumza leo Julai 17 jijini Dodoma wakati akielezea  utekelezaji  na mwelekeo wa wa majukumu ya Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Eliakim Maswi amesema wamezifungia kampuni kadhaa kufuatia makosa mbalimbali ikiwemo ya udanganyifu wa kugushi nyaraka za  taarifa za fedha za benki, na taarifa za malipo ya awali ya benki.

Kadhalika Maswi amesema mikakati iliyopo kwa Mamlaka hiyo kwa sasa ni   kuboresha  tatizo la  ununuuzi wa Umma liwe ni suala la  uwazi  ili kusiwe na mianya ya rushwa.

Ukosefu wa uwazi  katika  mchakato wa ununuuzi wa Umma kunasababisha changamoto za upatikanaji wa taarifa za zabuni, thamani ya mkataba na kusababisha ukosefu na uaminifu na imani kwa Taasisi za Umma pia hata wananchi wanakosa imani kwa Serikali kutokana na matumizi yasiyoeleweka

Waandishi mkiwa watafiti Wazuri mtaona kwamba kuna tatizo kubwa sana kwenye matumizi ya hela za Umma kuna wakati mwingine sisi hatufukirii kusema kwamba ile ni hela ya Umma ilindwe, ndio kwanza  wengine wanasema hiyo hela ya Serikali tu sasa nani anapaswa kuilinda ni mimi na wewe

Maswi.

Maswi amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi  Bilion 40 kwa PPRA ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo na kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka hiyo.

Hata hivyo Serikali imekuja na Mfuko mpya wa ununuuzi wa Umma kwa njia ya kielektroniki (NeST)  kufuatia  Serikali kutumia fedha nyingi zinazoidhinishwa kwenye bajeti kwaajili ya ununuuzi wa bidhaa, kandarasi za ujenzi na huduma  kuzingatia matakwa  ya Sheria ya ununuuzi wa Umma sura 410.

PPRA ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha sheria ya ununuuzi wa Umma sura namba 410 ambapo  malengo ya kuanzishwa kwake  ni  kuhakikisha  upatikanaji wa thamani ya Fedha katika ununuzi na ugavi , kuhakikisha uzingatiaji wa haki, ushindani uwazi uendelevu uwajibikaji matumizi mazuri ya Fedha ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi.



 

Post a Comment

0 Comments