KUFUATIA mabadiliko ya tabia nchi yanayoonesha kuathiri Mikoa ya Dodoma na Singida katika Uzalishaji wa mazao ya Kilimo, mifugo, na uvuvi Serikali imekuja na mbinu ambayo itaiwezesha Mikoa hiyo kuhimili mabadiliko hayo.
Aidha mbinu hizo ni pamoja na namna ya kuhifadhi maji na udongo mashambani zikijumuisha matumizi ya makingamaji, kilimo cha mbegu tisa na jembe la mzambia, kuzalisha mazao yanayotumia maji kwa ufanisi (Mtama na alizeti) uzalishaji wa malisho kwaajili ya mifugo, hifadhi ya misitu na upandaji wa miti matumizi ya nishati mbadala jua umeme na gesi kwaajili ya kupikia.
Hayo yamesemwa leo Julai 31, Jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea sherehe na maonesho ya nane nane kanda ya kati.
Maonesho hata yatatumika kuhamasisha vijana kujishughulisha na shughuli za Kilimo mifugo na uvuvi, Halmashauri zitahamasisha vijana waliofanikiwa kuja kwenye maonesho kutoa ushuhuda wa namna shughuli zao zilivyowanufaisha
Kadhalika maonesho hayo kwa mwaka huku makampuni na Watu binafsi wataleta Teknolojia za kisasa katika Kilimo na ufugaji bora, ambapo maonesho ya nanenane 2023 yatahusisha matukio muhimu na makongamano yanayoongeza wigo wa uzalishaji Bora.
0 Comments