JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limesema linajivunia mambo mbalimbali ikiwemo ongezeko la vijana wanaojiunga na Jeshi kwa mujibu wa sheria kutoka vijana 26,000 mwaka 2022/2023 hadi 52,119 mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54.
Aidha limesema ongezeko hilo limepatikana kutokana na jitihada za kuliwezesha jeshi hilo ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024, kiasi cha Shilingi Bilioni 9.96 kimetengwa ili kuendeleza azma ya kuboresha na kujenga miundombinu makambini.
Akieleza utekelezaji wa majukumu ya JKT na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024, leo Jijini Dodoma Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema azma ya serikali ni kuchukua vijana wote wanaomaliza kidato cha sita ili wahudhurie mafunzo ya lazima.
Meja Jenerali Mabele ameweka bayana mipango waliyonayo ya kuwaunganisha vijana wa Jeshi hilo na mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT), unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo.
JKT ilianzishwa rasmi mwaka 1963 ikiwa na majukumu mbalimbali ya msingi ikiwemo malezi ya vijana , ulinzi wa Taifa na uzalishaji mali
0 Comments