CANADA KUTOA DOLA MILIONI 50 KWAAJILI YA SHUGHULI MBALIMBALI ZA ELIMU TANZANIA.

 

📌RHODA SIMBA

SERIKALI ya Tanzania imeishukuru  Serikali  ya Canada kutangaza kuongeza Dollar milioni 50 kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za Elimu Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda  ametoa shukrani hizo leo  Julai 20, 2023 baada ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa na mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki Canada Mhe. Harjit S. Sajjan, kutangaza ongezeko hilo.

Amesema kuwa milioni 25 zitatumika kuwasaidia Wasichana kusoma na milioni 25 za zitatumika kuendeleza mafunzo ya Amali kwa vijana kuwawezesha kupata ajira.

Haya ni mafanikio ya Serikali kuendelea kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali na Rais wetu amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuimarisha mahusiano hayo

Prof. Mkenda.

Nae Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa na mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki la Canada Mhe. Harjit Sajjan amesema serikali ya nchi hiyo imekuwa Mshirika wa muda mrefu wa Tanzania katika sekta hiyo na imefanikiwa kuboresha viwango na upatikanaji wa Elimu kwa Shule zote pamoja na kusaidia jitihada mbalimbali za serikali.

Kwa kushirikiana na serikali tumewekeza katika mafunzo mathubuti kwa Walimu katika Vyuo 35 vya Ualimu" ambapo kwa miaka 14 Canada imetoa zaidi ya dollar za Canada milioni 250

Mhe. Sajjan.

Waziri huyo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuruhusu wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kurejea shuleni, ili kuwawezesha kupata maarifa na Ujuzi.

Ameongeza kuwa uwekezaji katika Elimu hasa mtoto wa kike hubadilisha jamii, huimarisha uchumi na kuchangia jamii kuwa imara zaidi. Hivyo nchi hiyo itaendelea kushirikiana kuendeleza sekta ya Elimu.

Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Taasisi ya Vyuo vya Canada Bi. Denise Amyot amesema program ya Uwezeshaji Kupitia Ujuzi (ESP) inalenga kuimarisha usawa wa kijinsia, inaunganisha Vyuo na Taasisi za Ufundi za Canada na nyingine kutoka nchi Washirika itaendeleza mbinu ya "Elimu Kwa ajira"



 

Post a Comment

0 Comments