BUWSSA YAELEZEA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UPOTEVU WA MAJI.

 ðŸ“ŒRHODA SIMBA

MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa mazingira Bunda Mkoani Mara (BUWSSA ) imeeleza kuwa  imeweka mkakati wa kupunguza upotevu wa Maji wa miaka mitatu ulioanza Mwaka 2020/2021 hadi Mwaka 2023/2024.

Hayo yamesemwa  leo Julai 20  Jijini Dodoma,  na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Esther Gilyoma wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya BUWSSA na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa fedha 2023/2024.

Upotevu wa Maji Bunda Mkoa wa Mara kwa mwaka 2022/2023 umefika asilimia 36 Mkakati huu ambao tunao najua utaenda kutokomeza kabisa upotevu wa maji katika Wilaya ya Bunda, hivyo wananchi waendelee kutunza miradi yetu ya maji

Gilyoma amesema Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imeandaa andiko la mradi kwaajili ya kukopa kuhakikisha upotevu wa Maji unapungua kwa kiasi kikubwa zaidi.

Tumeandaa andiko kwaajili ya kukopa fedha kiasi cha Shilingi 815,000,0000 ili upotevu wa maji upungue kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024

Gilyoma

Hata hivyo amesema Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Bunda haina huduma ya Majitaka, hivyo Magari ya Watu binafsi ambayo yanasimamiwa na halmashauri ya Mji wa Bunda ndiyo yatatumika katika kutoa huduma.

 

Post a Comment

0 Comments