HALMASHAURI kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma imekiri kuwa
inatambua siku kumi za ziara ya Katibu mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo zimeleta
majawabu ya matatizo na kero mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwatatiza wana
Dodoma kwa mda mrefu.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dodoma Pili
Mbanga amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akitoa tamko la Halmashauri
kuu ya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma kumpongeza Daniel Chongolo Katibu
mkuu wa chama hicho kwa ziara yake na wajumbe wa Sekretarieti ya NEC-CCM Taifa,
majimbo ya mkoa wa Dodoma kuanzia Juni 15 hadi 25,2023.
Mbanga amesema kuwa Katika ziara hiyo iliyoanzia Jimbo la
Mpwapwa Kisha Kibakwe, Kongwa, Chamwino, Mvumi, Kondoa Vijijini, Kondoa Mjini, Chemba,Bahi
na kuhitimisha na Jimbo la Dodoma Mjini kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara
Katibu mkuu alipokea taarifa ya utendaji wa kazi ya Chama Cha Mapinduzi mkoa, pia
alipokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2020-2025
kutoka kwa kamisa wa CCM mkoa wa Dodoma.
Aidha amesema kuwa Katibu mkuu alikagua na kutembelea
miradi thelathini na moja ambapo miradi ishirini na nane ni ya Serikali na
miradi mitatu ya Chama.
Kote alikopita katika miradi hiyo Katibu mkuu alitoa maelekezo mbalimbali kwa majimbo yote kumi ambapo mengine yalifanyiwa kazi papo kwa papo na mengine alielekeza muda wa kutekelezwa
Mbanga
Kwa upande wa Bahi na Chemba, Mbanga amesema kuwa
maelekezo yameanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na usimikaji nguzo za Umeme
kwenda kwenye kisima cha maji sambamba na kuimarisha usimamizi kwa mkandarasi.
Katika hatua nyingine Katibu mkuu alielekeza kuharakisha
zoezi la malipo ya kifuta jasho na swala la ardhi kwa wahanga wanyamapori
wakali Wilaya ya Kondoa ambapo jumla ya wahanga 451 walioharibiwa mazao yao, waliojeruhiwa
na wengine kuuwawa watalipwa kiasi Cha shilingi 130,475,000/=
Hata hivyo Mbanga ameongeza kuwa Halmashauri kuu ya Chama
Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma imeridhishwa na kifurahishwa na jitihada kubwa
zinazofanywa na Daniel Chongolo katika kuimarisha uhai wa Chama, kusimamia
utekelezaji wa ilani, kusikiliza na kupokea kero za wananchi Pamoja na kutoa
maelekezo kwa watendaji wa Serikali kwenye maeneo yote ambayo yanakutwa na
changamoto kwa Dodoma na sehemu nyingine.
0 Comments