KLABU ya
Yanga imepongezwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa kuchangia chupa 627 za
damu kwa mwaka 2023 huku akitoa wito kwa timu zingine kuiga mfano huo.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Juni 14, Jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani. Amesema Klabu ya Yanga imefanya jambo kubwa na la kiungwana kwa kuchangia chupa 627.
Napenda niwapongeze Yanga kupitia Rais Injinia Hersi Said kwa kuchangia chupa hizi za damu, mimi ni Simba lakini kama mngeshinda kule Algeria ningehamia Yanga.
Mheshimiwa Nyongo (Stanslaus) Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Ukimwi tunapigwa hadi kwenye damu? tunatakiwa kujipanga msimu ujao
Waziri Ummy
Klabu hiyo ambayo iliwakilishwa na Rais Injinia Hersi Said amepokea Cheti na Tuzo kwa kuchangia chupa hizo za Damu.
Naye Rais wa Timu ya Yanga Injinia Hersi Said amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kuchangia chupa hizo na kusema kuwa klabu hiyo itaendelea kuchangia damu lengo likiwa ni kuokoa watanzania wenye changamoto ya damu.
0 Comments