WAZIRI NDUMBARO:JUKWAA LA HAKI MWANAMKE NI ENDELEVU NA LINA MIFUMO IMARA KITUENDAJI.

 ðŸ“ŒJASMINE SHAMWEPU

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt, Damas Ndumbaro amesema jukwaa la Haki Mwanamke ni jukwaa endelevu ambalo limetengenezewa mifumo imara ya kiutendaji na litajishughulisha na maeneo mbalimbali ya utoaji haki nchini.

Hayo amezungumza leo Jijini  Dodoma wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo ambapo Waziri Ndumbaro amesema maandalizi ya upatikanaji  wa jukwaa hilo limepitia michakato mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na malengo ambayo yatamnufaisha mwanamke moja kwa moja.

Amesema maeneo hayo ni pamoja na eneo la haki kwa mujibu wa sheria, haki za kiuchumi, haki za kijamii, haki za kimazingira na haki za kisiasa.

Jukwaa hili litaendeshwa kwa mfumo rasmi ikiwa ni pamoja na kuwa na kamati mbalimbali za kiutendaji, Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Haki Mwanamke, Kamati ya Sekretariati, Kamati ya Uratibu Serikalini na Taasisi zisizokuwa za Kiserikali

Dkt Ndumbaro.

Amesema Serikali katika kulinda haki za Mwanamke itazingatia matakwa ya Katiba, Mikataba ya Kimataifa na Kikanda, Sheria mbalimbali za nchi Kanuni zilizopo, taratibu walizojiwekea na maelekezo mbalimbali ya Viongozi wa Serikali.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalum, Mwanaidi Ali Khamis amesema wanawake wamekuwa kimya pindi wanapokumbana na changamoto za maisha hivyo jukwaa hilo litahakikisha wanapata haki zao.

Naye Wakili wa Serikali Ester Msambazi ameeleza kuwa ukatili bado upo kwa wanawake kwakuwa mfumo wa haki haujamuwezesha kupata haki kwa wakati hivyo kupitia jukwaa hilo watahakikisha suala hilo linawafikia kwa wakati.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo amesema wanawake hukosa haki kwa sababu ya ukosefu wa uelewa hivyo kupitia jukwaa hilo kila mdau atatimiza wajibu wake ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa na wanapata haki zao.



 

 

 

Post a Comment

0 Comments