WAZIRI
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee, Watoto na Makundi Maalumu Mh. Dorothy
Gwajima amewataka wazazi na walezi
kulinda watoto wao katika kutumia mitandao ya kijamii vizuri bila kuvuka Maadili yanayotakiwa
katika Jamii.
Ametoa
kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizindua maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
duniani iliyofanyika leo na kauli mbiu ikiwa ni " Zingatia usalama wa
mtoto katika ulimwengu wa kidigitali" ambapo kauli hiyo ililenga kumuondoa
mtoto katika utumizi mbaya wa mitandao ya kijamii yaani kidigitali.
Dorothy
amesema wazazi, walezi na serikali wanashirikiana kikamilifu katika kulinda watoto ambapo kwasasa wana Mabaraza
takribani 592 na madawati ya kijinsia 1584 ambayo yanajiusisha na masuala ya
kijinsia nchini.
"Katika
siku ya Leo ni siku ambayo tunajumuika
kukumbuka watoto elfu mbili (2000) waliopoteza maisha katika kupigania haki yao ya elimu huko Afrika kusini
walikuwa wakidai haki zao za msingi hivyo tuwakumbuke watoto hao.
Sasa hivi asilimia kubwa ya watoto wamekuwa wakishiriki katika mitandao ya kijamii kwahiyo ni vema kutumia mitandao ya kijamii vizuri na katika mambo ya misingi wazazi tusaidiane katika hili kumlinda mtoto wa Afrika Dhidi ya matumizi wa mitandao isiyostahiki katika jamii.
Gwajima.
Kwa
upande wake Askari wa ulinzi na usalama Yusufu Kigoma amesema anashirikiana na
Jeshi la polisi katika kumtetea mtoto ambapo ametoa wimbo wa kumueshimu mtoto kwa
neno la “Don't touch my body” akimanisha kuweka marufuku kwa mtoto wa kike kushikwa
viungo vyao vya mwili.
Kwa mtoto ambae atafanyiwa kitendo cha ukatili akiniona mimi au Kiongozi yeyote hata kama ni Mheshimiwa Gwajima au mtu mwenye uwezo wa kusaidia mwambie ukatili uliofanyiwa apeleke taarifa katika dawati la jinsia utasaidiwa shida yako .
Pia jeshi la polisi liko makini katika kumlinda mtoto wa kike Dhidi ya ndoa za utotoni pia na watoto wote wakiwemo wa kiume katika kuhakikisha tunapokea ksei zao na kuzipeleka sehemu inayotakiwa na kutoa adhabu kwa wahusika hivyo hatulali tukishirikiana na viongozi wetu
Yusufu
0 Comments