WAZAZI
wenye watoto walemavu wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kupata
elimu kama watoto wengine na si kuwaficha nyumbani.
Wito
huo umetolewa Juni 24, 2023 wilayani Bahi mkoani Dodoma na Mratibu wa Mradi wa
Elimu Jumuishi Janey Mgidange wakati akiongea na wazazi hao wilayani humo,
ambapo amesema kitendo cha kuwaficha nyumbani kinawanyima haki yao ya msingi ya
kupata elimu.
Wazazi tujitahidi katika hili. Langu kubwa na la msingi wazazi mhakikishe mtoto mwenye ulemavu anaenda shule. Ni wajibu wako kwa sababu umemleta mwenyewe, kwa hiyo unatakiwa ufuate Sheria ya Tanzani inasema nini anapofikisha umri wa miaka minne aende shule haijalishi ni mlemavu ama si mlemavu.
Kuna mtu mwingine anasema sasa yule kiziwi anawezaje kwenda shule. Ulimpeleka shule ukaambiwa kwamba hakuna anayemuweza? Na kama ulimpeleka shule njoo uniambie ni wapi. Au kama haoni ulimpeleka shule wakasema sisi hatuwezi kumfundisha? Na kama ulimpeleka huyo mtoto njoo umuone hata Mtendaji wa Kata atatuambia ni shule gani na ni mwalimu nani ambaye amemkata huyo mtoto.
Janey.
Diwani
wa Kata ya Bahi wilayani humo Augustino Ndonu amesema baadhi ya watu wamekuwa
na dhana ya kwamba mtoto anapozaliwa na ulemavu hapaswi kusoma jambo ambalo si
kweli.
Hivi mtoto wako mwenye ulemavu ukimfungia ndani utakuwa umemfanyia ukatili au unampenda? Bila shaka unamchukia. Na haya mambo yanafanyika hapa, wazazi mnachukua hatua gani?
Diwani
Katibu
wa wazazi wenye watoto walemavu Rajab Mohamed wilayani humo amesema, wapo
baadhi ya wazazi ambao wameshindwa kukubaliana na hali ya watoto wao kuwa ni
walemavu, hali ambayo imepelekea kuanza kuwabagua wao wenyewe.
Kutokuubali kunamfanya mzazi mwenyewe kumnyanyapaa mtoto. Hata wakati ambao ameweka chakula anamuwekea mlemavu peke yake na hawa wengine peke yao.
Rajab.
Naye
Maria Emanuel mzazi mwenye mtoto mlemavu ametumia hadhara hiyo kuwaelimisha wazazi kujua umuhimu wa kuwapenda na kuwathamini watoto wenye
ulemavu na si kuwabagua.
Kina mama wenzangu mimi ni mzazi kama nyie nina mtoto mlemavu. Mtoto wangu sikutaka kumuweka ndani nilimuweka nje akaenda shule . Nawaomba wazazi hawa watoto ni sadaka kwa mwenyezi Mungu tusiwafiche.
Maria.
Ingawa
Malengo ya Maendeleo Endelevu yanahimiza kuwa hakuna mtoto anayepaswa kuachwa
nyumba, utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF
unaonesha kuwa kati ya watoto milioni 240 wenye ulemavu duniani, nusu
hawajawahi kuhudhuria shule.
Utafiti
huo pia unaonesha, takriban theluthi moja hawapati chakula bora na cha kutosha
na pia watoto wenye ulemavu wanawakilishwa kwa njia isiyo sawa na wengi wao
wanaachwa nyuma.
0 Comments