WAZIRI
wa nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh. George Boniphace Simbachawene amezitaka Taasisi
za umma, Wizara na mamlaka zote nchini
kusimamia mkataba wa utumishi wa umma kwa wateja ikiwemo utekelezaji wa huduma
za kijamii kama maji, umeme, shule na afya
kwa kizingatia haki na usawa kwa wananchi.
Waziri
Simbachawene ameyasema hayo leo jijini
Dodoma kwenye mazimisho ya kilele cha wiki ya utumishi wa umma zoezi ambalo
limeenda sanjali na uzinduzi wa mikataba ya utumishi wa umma
Amesema
uzalendo ni kutekeleza jukumu ambalo umepangiwa kwa ufanisi mkubwa wa kutaka
kazi hiyo ifanyike kwa ubora zaidi huku akieleza namna pekee ambayo wananchi
wanatumia kama kipimo kwa serikali ni huduma za kijamii zinapowafikia
Taasisi na mamalaka mtimize majuku yenu kwa kuzingatia maadili, usawa, na nidhamu katika utendaji kazi wenu na sio kwamba wewe kwakuwa upo unasimamia Sheria basi uwe juu ya Sheria kwamaana kazi ya Sheria ni kutimiza haki
Mjue kuwa mnalo jukumu la kuhakikisha kuwa unafanya kazi kwa kujali wateja na sio kuwa na dharau katika ofisi zenu ukiwa mtumishi wa umma usimame katika haki na usawa
Simbachawene
Amesema
mwaka jana alitoa maelekezo kwa taasisi za
umma kutekeleza mkataba wa huduma
kwa wateja ambapo imeleta mafanikio mbalimbali ikiwemo kuongeza uwajibikaji kwa
watumishi wa umma
Mkataba wa watumishi wa umma unaweza kuona Sasa umeleta mafanikio na mabadiliko makubwa kwa watumishi kwanza imeongeza uwajibikaji na nidhamu ya kufanya kazi, lakini pia imeweza kubadilisha mtazamo wa kufanya kazi kwa mazoea pia fikra za watumishi wa umma kwa wateja katika idara na taasisi mbalimbali nchini, hivyo sasa wanafanyakazi kwa usawa na nidhamu kubwa
Simbachawene
Hata
hivyo Naibu Katibu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Sospeter Mtwela emeeleza mkataba wa huduma kwa wateja ni makubaliano
kimandishi ambayo mtumishi wa umma
anakula kiapo cha kusimamia na kulinda Mikataba katika utendaji wake wa kazi
bila kuvunja Sheria
Ninaahidi mikoa yote nchini pamoja na serikali za mitaa nchini kote kuandaa mikataba na kusimamia mikataba kwa watumishi wa umma katika kutekeleza utekelezaji ambao umeandikwa kisheria lakini tujali majukumu ambayo tunatakiwa kuyafanya
Nikiri kwamba bado mikataba ya watumishi wa umma katika ofisi za serikali ya mitaa bado hatujazingatia katika ngazi ya mikoa na mitaa hivyo tunaenda kutekeleza hilo
Mtwela
Kwa
upande wake Katibu mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mh,
Juma Mkomi ametoa pongezi kwa tasisi zote zilizofanya vizuri katika utumishi wa
umma na ameongeza kuwa itaongeza chachu ya utendaji kazi katika utendaji na
uhamasishaji taasisi na mamlaka mbalimbali ili kuongeza nguvu katika
utekelezaji wa kazi
Takribani taasisi 34 zitazinduliwa na taasisi ambazo zimefanya vizuri kupewa tuzo na itakuwa chachu katika kujipanga zaidi na maazimisho ya mwaka kesho tunataka tuone jitihada za serikali zinawanufaisha wananchi
Mikataba inayozinduliwa katika kilele cha maazimisho ya watumishi wa umma ni ahadi kimaandishi ambayo mtumishi wa umma humuwezesha mteja kufahamu fursa za taasisi za umma na njia zitakazomwezesha mteja
Mkomi
Wiki
ya watumishi wa umma hufanyika kila mwaka ifikapo Juni 16 hadi Juni 23 lengo na
madhumuni ya mazimisho hayo ni kuhakikisha huduma za serikali kwa wananchi
zinawafikia na kuwanufaisha watu wote nchini. Kaulimbiu katika kilele Cha
maazimisho ya wiki ya watumishi wa umma kwa mwaka huu inasema “Mafanikio kwa
eneo huru la biashara barani Afrika inahitaji usimamizi wa watumishi wa umma”
0 Comments