NAIBU
Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma mjini Mh.Antony Mavunde amewataka wanawake
wajasiriamali jijini Dodoma kuchangamkia fursa katika biashara pamoja na kuongeza
ujuzi ikiwemo kushiriki semina mbalimbali ili kujifunza na Kuongeza chachu
katika kuinua uchumi wa viwanda
Kauli
hiyo ameitoa Leo juni 9 jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya Wanawake
wanaweza maarufu kama (SheCanDoIt) yenye lengo la kumuinua mwanamke kiuchumi na
kumtoa katika biashara ndogo hadi kumiliki kiwanda kutokana na kuzingatia
mafunzo ya semina.
Amesema serikali imetenga pesa kwaajili ya
kujenga Jiji la Dodoma hivyo fursa za biashara zitaongezeka kutokana na mji
kupanuka na hii itawanufaisha wajasiriamali.
Lakini
pia serikali imeanzisha Sera itakayowanufaisha wanawake, watoto na makundi
maalumu kwani serikali ina sheria ya asilimia 30 ya wanawake kujihusisha katika
frusa hizo za ajira
Wanawake wajasiriamali serikali kupitia Sheria hizo inawapenda sana na inahitaji mfike mbali katika kuanzisha biashara na kuja kufikia uchumi wa viwanda na ndio maana bado fursa zinaongezeka na kuwalenga
Ambapo ajira za vijana wazee na watu wenye ulemavu wakiwemo wakina mama kuhusika katika kupata na kuchangamkia frusa za ajira ambapo ni moja ya malengo ya serikali katika kukuza ajira kwenu
Mh Mavunde.
Kwa sasa wajasiriamali wameweza kupata wawekezaji ambao wanawainua wanawake katika kukuza biashara nayo ni Bank na Makundi ya wanawake katika kukuza na kuanzisha biashara hivyo changamkieni fursa
Ni vibaya kwa mjasiriamali yeyote kuchukua mkopo mkubwa ambao upo kinyume na biashara yake na hiyo inakuja baadaa ya kuingizwa katika ushawishi wa kuchukuwa mkopo usio na malengo.
Bi.Festa.
Naye mjasiriamali wa kujitegemea Bi. Zuhura Mkweo amesema semina hii imekuwa na faida kwake ambapo ataenda kuwa msimamizi bora wa biashara yake ya kuuza matunda na juisi kutokana na elimu aliyopatiwa leo
Nimejua jinsi ya kuongeza mtaji kutoka Benki yaani mkopo pia nimepata akili mpya ya kwenda kutatua changamoto baadhi katika biashara yangu kupitia hapo nitaweza kuongeza mtaji kuwa mkubwa zaidi.
Pia ni vyema kuendelea kupenda kazi yetu tunayoifanya kwa ababu serikali yetu inatuunga mkono ili kufikia malengo makubwa kupitia ujasiriamali wa wafanyabiashara wote tukiwemo na sisi wanawake
Zuhura.
0 Comments