KIWANDA cha kusindika kimea (MALT) mkani Kilimanjaro kuanza kufanya kazi Machi 2024 huku ajira 17500 zinatarajiwa kupatikana kwa wakulima wa shayiri .
Waziri wa Kilimo Hussen Bashe ameyasema hayo wakati wa makubaliano ya kimkataba kati ya kiwanda cha Kilimanjaro ambapo wanalenga kupunguza uagizaji wa zao la shayiri kutoka nje .
Waziri Bashe amesema makubalinao hayo yamefanywa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) na unatarajia kufikia gharama ya shilingi bilioni 90 .
Hii ni neema wakulima ongeza uzalishaji zaidi kwani mmepata soko la uhakika
Waziri Bashe
Naye Mkurugenzi wa uendeshaji TBL Richmond Raymond amesema kiwanda hicho kitawezesha serikali kupata mapoto chiringi Bilioni 226 na kitanunua shayir moja Kwa moja Kwa wakulima
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzania Breweries Limited (TBL) Jose Moran amesema wamejidhatiti kununua mazao ya wakulima kwa bei itakayowapa ari ya kuzalisha zaidi na kuongeza thamani.
Niombee ushirikiano kwa wakulima katika uzalishaji wa shayiri kuwa mkubwa kwani tunategemea kuongeza nguvu ya uzalishaji wa vinywaji vitokanavyo na shayiri na kukuza soko.
0 Comments