SERIKALI
imesema kuwa Vijiji vyote ambavyo vipo kwenye Mradi wa REA awamu ya 3 mzunguko
wa pili vitakamilika ifikapo Disemba mwaka huu 2023.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itapelekea umeme kwenye vijiji vya kata ya Shizuvi ambavyo ni sehemu ya REA awamu ya 3 mzunguko wa pili?
Vijiji vyote ambavyo vipo kwenye mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili vitakamilika ifikapo Disemba mwaka huu 2023
Nimuhakikishie
Mheshimiwa Orani Njeza kwamba vijiji hivyo pia katika kata hizo vitakuwa
vimefikiwa umeme kabla ya Disemba mwaka huu,"amesema Naibu Byabato.
0 Comments