MWENYEKITI
wa Shirika lisilo la kiserikali la (Kingdom Leadership Network) yaani mtandao
wa ufalme na uongozi nchini Bw. Isaac Makala amewataka vijana jijini Dodoma
kuhudhuria mkutano wa fursa kwa vijana unaojulikana kama Tanzania National Breakfast mkutano wa kisiasa pia kusisitiza uongozi wa
serikali kiroho zaidi na wenye hofu ya mwenyezi Mungu
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Bw. Isaac Makala amesema vijana
wanatakiwa kuona na kuchangamkia fursa ili kujiinua kiuchumi kwa manufaa ya taifa
na uchumi wa mtu mmoja mmoja
Amesema
mkutano utakuwa wa siku mbili kuanzia Ijumaa (Juni 23) na Jumamosi (Juni 24)
saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini
hapo ambapo viongozi mbali mbali kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
watakuwepo ili kutoa elimu kwa vijana
Waziri mstaafu Mizengo Pinda atakuwepo lakini pia Mkuu wa Mkoa na mawaziri mbalimbali watakuwepo kutoka ndani ya nchi hii inaonesha nguvu ya viongozi kwa taifa
Lakini pia tutakuwa Prof. Lumumba kutoka Nigeria lakini pia Dkt Paul Henenche, mchungaji mwenye kanisa kubwa zaidi kuliko yote hii ni katika kuhakikisha vijana wanahamasika na kujifunza kuelekea katika ubilionea mpya pia viongozi wengi watakuwepo kutoka Marekani
Makala
Naye
Geofrey Simbei, Mkurugenzi wa Taasisi binafsi Tanzania amesema wametengeneza
majukwaa makubwa nchini na katika bara la Afrika ambapo inajumuisha nchi 15
katika sekta ya Kilimo wanataka kuona Afrika inauza sana mazao ya kilimo katika
nchi ya Marekani
Korosho inazalishwa sana Tanzania lakini wanaoonekana wanauza korosho ni Vietinam kwa maana wao wanachukua korosho kuroka kwetu baadae wao wanaichambua na kutoa gamba la nje kisha wanaifungasha kwenye pakiti na kuuza Marekani,
Tunataka kesho tukae na vijana halafu kesho kutwa tunaenda kukaa na National Player Breakfast Tanzania ili tuweze kuwa wakubwa katika kuzalisha na kufanya biashara ili kuweza kuinua uchumi wetu
Simbei
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa makanisa Tanzania CCT Mchungaji Moses Matonya amewakaribisha
waumini wa dini zote nchini pamoja na mabaraza ya maaskofu kuhudhuria
kushirikiana na Kingdom Leadership Network kusukuma hamasa na kuona ni namna
gani wanaweza kunufaika kiuchumi na kumshukuru mwenyezi Mungu
Kwa niaba ya umoja wa makanisa Tanzania niwaalike wachungaji, maaskofu, na mashekhe, kujumuika na kunufaika na uwekezaji tuweze kujikwamua kiuchumi kwa maana vyote mwenyezi Mungu ameviweka hapa
Karibuni wote tuweze kuona ni fursa zipi zinaweza kutunufaisha sisi na makanisa yetu pamoja na waumini wote kwani ni fursa zetu wenyewe karibuni Jakaya Kikwete
Mchungaji Matonya
Hata
hivyo Arnold Mtewele Mkurugenzi wa Ukumbi wa Jakaya Kikwete ametoa wito kwa
vijana wote jijini Dodoma kuhudhuria mkutano wa fursa kwa vijana ili waweze
kujifunza kwani kutakuwa na viongozi wa dini ambao watanena kwaajili yao hivyo
wasiache kufika kwani inalenga kutathimini maadili kwa viongozi
Ulinzi upo wa kutosha hapa Jakaya tumehakikisha mali zote zipo salama wala hakutakuwa na shida yeyote maeneo yote ya kuegesha magari yapo salama hivyo vijana karibuni sana tujifunze
Kama mnavyojua ukumbi wa Jakaya ni mdogo hivyo hakutakuwa na nafasi ya kutosha cha kuwashauri muwahi kufika mapema mara tu ukumbi ukijaa hakutakuwa na nafasi nyingine tunawakaribisha sana kuhudhuria mkutano
Mtewele
0 Comments