VIJANA
Jijini Dodoma wametakiwa kujenga utamaduni wa kujifunza vitu tofauti katika
maisha ili waweze kujiajiri wenyewe na sio kubaki nyumbani au kuzurura mtaani
bila kazi badala yake watafute ujuzi na elimu itakayosaidia kuwaingizia kipato
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Mzee Ally Juma wakati akizungumza na CPC
Blog kuhusu ajira yake ya kinyozi kwa kutumia nyembe kitu ambacho ni tofauti na siku hizi kutokana na kukua kwa
Sayansi na Teknolojia
Amesema
kazi hiyo inampatia kipato na kusaidia kujikimu kimaisha kwani ni kazi ambayo
ameifanya zaidi ya miaka ishirini(20) na imekua kazi yake pendwa kila siku
kulingana na kipato anachokipata
Nilianza na mtaji mdogo kwenye biashara hii wala haikuhitaji pesa nyingi kuanzisha, nilichukua kiti cha nyumbani, maji, na nyembe na kuanzisha kituo chini ya huu mti, nafanya hivi kwa sababu zamani sisi tulitumia mkasi na nyembe kunyolewa na wazazi wetu hivyo nilijifunza kutoka kwao
Wateja wangu wengi ni wazee na vijana wanajitokeza kidogo sana nadhani kutokana na mabadiliko ya teknolojia hivyo niwaombe vijana wapende kujifunza vitu mbalimbali katika maisha ili waweze kujiajiri wenyewe huu ni ujuzu kama ujuzi mwingine
Juma
Kwa
upande wake Hamis Ramadhan amesema anajisikia furaha kubwa kuona wanaenzi tamaduni za Afrika japo kuna mabadiliko makubwa
ya Sayansi na teknolojia lakini mzee Ally yeye anarudisha enzi za mababu
Njia hii ni salama zaidi kulinganisha na njia ya saloon kwani inasaidi kupunguza kuenea kwa magonjwa maana kila mmoja anatumia wembe wake tofauti na mashine wembe mmoja watu zaidi ya mmoja,
Binafsi nafurahishwa na gharama ya unyoaji wa nywele shillingi elfu moja nanyoa kwa usalama zaidi tofauti na saloon kama unavyojua binadamu tuna changamoto za kiafya, magonjwa na mambo mengi, sasa hii ni njia salama kwangu
Ramadhani
Naye
Geofrey Daniel kinyozi wa saluni za kisasa Soko la Machinga Complex Jijini
dodoma amesema ni kweli kuhusu tafiti
zinaonesha unyoaji wa nywele usiozingatia usalama wa afya za wateja katika
saluni mbalimbali unatishia hali ya afya na kupelekea kuenea kwa magonjwa ya
kuambukiza hasa homa ya ini na ngozi wakati wa kunjoa mashine za umeme
zinazotumika huweza kusababisha michubuko midogo midogo kichwani hasa kwa wanao
chonga nywele
Njia hii ya saluni inahitaji umakini wa hali ya juu kwa mnyoaji ili kuhakikisha mteja anakuwa salama, kwanza lazima uwe na mashine zaidi ya moja lakini pia usafi wa mteja baada ya kunyolewa lazima kumpaka spiriti kwaajili ya kuua vijidudu vya magonjwa
Saluni inahitaji gharama tofauti na kunyoa kwa wembe kwani gharama yake ni ndogo tena ni salama zaidi kuliko njia hii ya saluni ili kuepuka maambukizi ya magonjwa, niwashauri vijana wenzangu kizingatia kanuki za unyoaji na umakini kwa ajili ya kulinda afya zetu na wateja kiujumla
Daniel
0 Comments